Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 22:3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

3 Mimi ni mtu wa Kiyahudi, nalizaliwa Tarso, mji wa Kilikia, nikalelewa katika niji huu miguumi pa Gamaliel, nikafundishwa sharia ya baba zetu kwa usahihi, nikawa mtu wa ijtihadi kwa Mungu kama ninyi nyote mlivyo leo hivi:

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 “Mimi ni Myahudi, mzaliwa wa Tarso katika Kilikia. Lakini nililelewa papa hapa mjini Yerusalemu chini ya mkufunzi Gamalieli. Nilifundishwa kufuata kwa uthabiti sheria ya wazee wetu. Nilijitolea kwa moyo wote kwa Mungu kama nyinyi wenyewe mlivyo hivi leo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 “Mimi ni Myahudi, mzaliwa wa Tarso katika Kilikia. Lakini nililelewa papa hapa mjini Yerusalemu chini ya mkufunzi Gamalieli. Nilifundishwa kufuata kwa uthabiti sheria ya wazee wetu. Nilijitolea kwa moyo wote kwa Mungu kama nyinyi wenyewe mlivyo hivi leo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 “Mimi ni Myahudi, mzaliwa wa Tarso katika Kilikia. Lakini nililelewa papa hapa mjini Yerusalemu chini ya mkufunzi Gamalieli. Nilifundishwa kufuata kwa uthabiti sheria ya wazee wetu. Nilijitolea kwa moyo wote kwa Mungu kama nyinyi wenyewe mlivyo hivi leo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 “Mimi ni Myahudi, niliyezaliwa Tarso huko Kilikia, lakini nimelelewa katika mji huu. Miguuni mwa Gamalieli, nilifundishwa kikamilifu katika sheria ya baba zetu, na nikawa mwenye juhudi kwa ajili ya Mungu kama nyote mlivyo leo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 “Mimi ni Myahudi, niliyezaliwa Tarso huko Kilikia, lakini nimelelewa katika mji huu. Miguuni mwa Gamalieli, nilifundishwa kikamilifu katika sheria ya baba zetu, na nikawa mwenye juhudi kwa ajili ya Mungu kama kila mmoja wenu alivyo leo.

Tazama sura Nakili




Matendo 22:3
27 Marejeleo ya Msalaba  

Nae alikuwa na ndugu mwanamke aitwae Mariamu, nae alikuwa ameketi miguuni pa Yesu, akasikia maneno yake.


Ikawa baada ya siku tatu, wakamwona hekaluni, ameketi kati ya waalimu, akiwasikiliza, na kuwauliza.


Wakatoka waone khabari iliyotokea. Wakamwendea Yesu, wakamwona yule mtu aliyetokwa na wale pepo ameketi migunni pa Yesu, amevaa nguo, ana akili zake: wakaogopa.


Barnabi tikatoka akaenda Tarso kumtafuta Saul: hatta alipokwisha kumwona akamleta Antiokia.


Wakaandika hivi kwa mikono yao, Mitume na wazee na ndugu, kwa ndugu zetu walioko Antiokia na Shami na Kilikia, walio wa mataifa, salamu.


Akapita katika Shami na Kilikia akawatia moyo makanisa.


Nao waliposikia wakamhimidi Mungu, wakamwambia, Ndugu yetu, unaona kwamba Wayahudi walioamini walivyo elfu nyingi, nao wote wana wivu sana kwa ajili ya torati.


Paolo akasema, Mimi ni mtu wa Kiyahudi, mtu wa Tarso, mji wa Kilikia, mwenyeji wa mji usio mnyonge. Nakuomba, nipe rukhusa niseme na wenyeji hawa.


Alipoarifiwa ya kuwa ni mtu wa Kilikia, akasema,


Paolo alipotambua ya kuwa sehemu moja ni Mafarisayo, na sehemu ya pili Masadukayo, akapaaza sauti yake katika ile baraza, Ndugu zangu, mimi ni Farisayo, mwana wa Farisayo: mimi ninahukumiwa kwa ajili ya tumaini la ufufuo wa wafu.


wakinijua sana tangu mwanzo, kama wakipenda kushuhudia, ya kwamba nalikuwa Farisayo kwa kuifuata madhehebu ya dini yetu iliyo sahihi kabisa.


Kweli, mimi mwenyewe naliona ndani ya nafsi yangu kwamba yanipasa kutenda mambo mengi yaliyopingamana na jina lake Yesu Mnazareti;


Lakini mtu mmoja, Farisayo, jina lake Gamaliel, mwalimu wa torati, mwenye kuheshimiwa na watu wote, akasimama katika baraza,


Lakini baadhi ya watu wa sunagogi lililokwitwa sunagogi la Malibertino, na la Wakurene na la Waiskanderia, na la wale wa Kilikia na Asia, wakaondoka wakajadiliana na Stefano:


LAKINI Saul, akizidi kutisha na kuwaza kuwaua wanafunzi wa Bwana, akamwendea kuhani mkuu,


Bwana akamwambia, Simama, enenda zako katika njia iitwayo Sawa, ukatafute ndani ya nyumba ya Yuda mtu jina lake Saul, wa Tarso: maana yuko anasali:


Lakini ndugu walipopata khabari wakamchukua hatta Kaisaria wakampeleka Tarso.


BASSI, nauliza. Mungu aliwasukumia mbali watu wake? Hasha! maana mimi nami ni Mwisraeli, mmoja wa wazao wa Ibrahimu, mtu wa kabila ya Benjamin.


Wao Waebrania? Na mimi. Wao Waisraeli? Na mimi. Wao uzao wa Ibrahimu? Na mimi.


nami nalitangulia katika dini ya Kiyahudi kuliko wengi walio hirimu zangu katika kabila yangu, nikajitahidi sana katika kushika mapokeo ya baba zangu.


Khalafu nalikwenda pande za Sham na Kilikia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo