Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 22:12 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

12 Bassi mtu mmoja, Anania, mcha Mungu kwa kuifuata sharia, aliyeshuhudiwa na Wayahudi wote waliokaa huko, akanijia, akasimama karibu nami, akaniambia, Ndugu, Saul, uone.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 “Huko kulikuwa na mtu mmoja aitwaye Anania, mtu mcha Mungu, mwenye kuitii sheria yetu na aliyeheshimika sana mbele ya Wayahudi waliokuwa wanaishi Damasko.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 “Huko kulikuwa na mtu mmoja aitwaye Anania, mtu mcha Mungu, mwenye kuitii sheria yetu na aliyeheshimika sana mbele ya Wayahudi waliokuwa wanaishi Damasko.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 “Huko kulikuwa na mtu mmoja aitwaye Anania, mtu mcha Mungu, mwenye kuitii sheria yetu na aliyeheshimika sana mbele ya Wayahudi waliokuwa wanaishi Damasko.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 “Mtu mmoja mcha Mungu, jina lake Anania, alikuja kuniona. Alizishika sana sheria zetu, na aliheshimiwa sana na Wayahudi walioishi huko Dameski.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 “Mtu mmoja mcha Mungu, jina lake Anania, alikuja kuniona. Alizishika sana sheria zetu, na aliheshimiwa sana na Wayahudi waliokuwa wakiishi huko Dameski.

Tazama sura Nakili




Matendo 22:12
10 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi kulikuwako mtu katika Yerusalemi, jina lake Sumeon; na yule mtu mwenye haki, mtawa, akitazamia faraja ya Israeli: na Roho Mtakatifu alikuwa pamoja nae.


Wakasema, Kornelio akida, mtu mwenye haki, mcha Mungu, aliye na sifa njema kwa taifa lote la Wayahudi, alionywa na malaika mtakatifu kutuma watu kwako, uende nyumbani kwake, apate kusikiliza maneno yako.


Wengine wakaamini, wakasuhubiana na Paolo na Sila; na Wayunani waliomcha Mungu, wengi sana, na wanawake wenye eheo si wachache.


Bassi ndugu, chagueni watu saba miongoni mwenu, walioshuhudiwa kuwa wema, illi tuwaweke juu ya jambo hili:


Watu watawa wakamzika Stefano, wakamfanyia maombolezo mengi.


kwa utukufu na aibu, kwa kunenwa vibaya na kunenwa vyema; kama wadanganyao, bali watu wa kweli;


Imempasa tena kushuhudiwa mazuri na watu walio nje; asitumbukie katika lawama na mtego wa Shetani.


Maana kwa hiyo wazee wetu walishuhudiwa.


Demetrio ameshuhudiwa na watu wote, tena na ile kweli yenyewe. Na sisi pia twashuhudu, nawe wajua ya kwamba ushuhuda wetu ni kweli.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo