Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Matendo 21:34 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

34 Wengine katika makutano wakapiga kelele wakisema hivi, na wengine hivi. Bassi alipokuwa hawezi kupata hakika ya khabari kwa sababu ya zile kelele, akatoa amri aletwe ndani ya ngome.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

34 Wengine katika lile kundi la watu walikuwa wanapayuka kitu hiki na wengine kitu kingine. Kwa sababu ya ghasia hiyo, mkuu wa jeshi hakufaulu kujua kisa kamili. Hivyo, aliamuru watu wake wampeleke Paulo ndani ya ngome.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

34 Wengine katika lile kundi la watu walikuwa wanapayuka kitu hiki na wengine kitu kingine. Kwa sababu ya ghasia hiyo, mkuu wa jeshi hakufaulu kujua kisa kamili. Hivyo, aliamuru watu wake wampeleke Paulo ndani ya ngome.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

34 Wengine katika lile kundi la watu walikuwa wanapayuka kitu hiki na wengine kitu kingine. Kwa sababu ya ghasia hiyo, mkuu wa jeshi hakufaulu kujua kisa kamili. Hivyo, aliamuru watu wake wampeleke Paulo ndani ya ngome.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

34 Baadhi ya watu katika umati ule wakapiga kelele, hawa wakisema hili na wengine lile. Yule jemadari alipoona kuwa hawezi kupata hakika ya habari kwa sababu ya taharuki, akaamuru Paulo apelekwe katika ngome ya jeshi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

34 Baadhi ya watu katika ule umati wakapiga kelele, hawa wakisema hili na wengine lile. Yule jemadari alipoona kuwa hawezi kupata hakika ya habari kwa sababu ya zile kelele, akaamuru Paulo apelekwe katika ngome ya jeshi.

Tazama sura Nakili

Matendo 21:34
8 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi wengine walikuwa wakilia hivi na wengine hivi: kwa maana ule mkutano umekwisha kuchafukachafuka, na walio wengi hawakuijua sababu ya kukusanyika kwao pamoja.

Na Paolo alipokuwa anaingizwa ndani ya ngome, akamwambia jemadari, Nina rukhusa nikuambie neno? Nae akasema, Je! unajua Kiyunani?

yule jemadari akaamuru aletwe ndani ya ngome, akisema aulizwe khabari zake kwa kupigwa, illi ajue sababu hatta wakampigia kelele namna hii.

Siku ya pili yake akitaka kujua hakika, ni kwa sababu gani ameshitakiwa na Wayahudi, akamfungua, akawaamuru makuhani wakuu na baraza yote waje. Akamleta Paolo chini, akamweka mbele yao.

Ugomvi mkubwa ulipotokea, yule jemadari akachelea Paolo asije akararuliwa nao, akaamuru askari washuke na kumpokonya mikononi mwao, na kumleta ndani ya ngome.

Mjomba wake Paolo akasikia khabari za kuotea kwao, akaenda akaingia ndani ya ngome akampasha Paolo khabari.

hatta assubuhi wakawaacha wale wapanda farasi waende pamoja nae, nao wakarudi zao ngomeni.

Nami sina neno la hakika la kumwandikia Bwana. Kwa hiyo nimemleta hapa mbele yenu, illi akiisha kuulizwa khabari zake, nipate neno la kuandika.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo