Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 21:33 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

33 Kiisha jemadari akakaribia, akamshika, akaamuru afungwe kwa minyororo miwili: akauliza, Nani huyu? tena, amefanya nini?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

33 Mkuu wa jeshi alimwendea Paulo, akamtia nguvuni na kuamuru afungwe minyororo miwili. Kisha akauliza, “Ni mtu gani huyu, na amefanya nini?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

33 Mkuu wa jeshi alimwendea Paulo, akamtia nguvuni na kuamuru afungwe minyororo miwili. Kisha akauliza, “Ni mtu gani huyu, na amefanya nini?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

33 Mkuu wa jeshi alimwendea Paulo, akamtia nguvuni na kuamuru afungwe minyororo miwili. Kisha akauliza, “Ni mtu gani huyu, na amefanya nini?”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

33 Yule jemadari akaja, akamkamata Paulo akaamuru afungwe kwa minyororo miwili. Akauliza yeye ni nani, na alikuwa amefanya nini.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

33 Yule jemadari akaja, akamkamata Paulo akaamuru afungwe kwa minyororo miwili. Akauliza yeye ni nani, na alikuwa amefanya nini.

Tazama sura Nakili




Matendo 21:33
18 Marejeleo ya Msalaba  

Hatta wakati Herode alipotaka kumtoa, usiku uleule. Petro alikuwa amelala kati ya askari wawili, amefungwa minyororo miwili: walinzi mbele ya mlango wakailinda gereza.


illa ya kuwa Roho Mtakatifu mji kwa mji hunishuhudia akisema, ya kwamba vifungo na mateso yaningoja.


Alipotufikia akautwaa mshipi wa Paolo akajifunga miguu na mikono, akasema, Roho Mtakatifu asema hivi, Hivyo ndivyo Wayahudi wa Yerusalemi watakavyomfunga mtu mwenye mshipi huu, nao watamtia katika mikono ya watu wa mataifa.


Bassi wale waliokuwa tayari kumwuliza wakaondoka wakamwacha. Na yule jemadari nae akaogopa, alipojua ya kuwa ni Mrumi, na kwa sababu amemfunga.


Siku ya pili yake akitaka kujua hakika, ni kwa sababu gani ameshitakiwa na Wayahudi, akamfungua, akawaamuru makuhani wakuu na baraza yote waje. Akamleta Paolo chini, akamweka mbele yao.


Nikawajibu kwamba sio desturi ya Warumi kumtoa mtu aliye yote auawe, kabla mtu yule aliyeshitakiwa hajaonana na washitaki wake uso kwa uso, na kupewa nafasi ya kujitetea katika mashitaka yake.


Paolo akamjibu, Namwomba Mungu kwamba ikiwa kwa machache au ikiwa kwa mengi si wewe tu illa na hao wote wanaonisikia leo wawe kama mimi pasipo vifungo hivi.


Bassi kwa ajili ya hayo, nimewaiteni mje kunitazama na kusema nami; kwa maana nimefungwa kwa mnyororo huu kwa ajili ya tumaini la Israeli.


kwayo ni mjumbe kifungoni; nipate ujasiri katika kunena jinsi nipaswavyo kusema.


kama ilivyo wajib wangu kufikiri haya juu yenu nyote; kwa sababu ninyi mmo moyoni mwangu; kwa kuwa katika kufungwa kwangu na katika kazi ya kuitetea Injili na kuithubutisha, ninyi nyote mmeshirikiana nami neema hii.


Bwana awape rehema walio wa uyumba ya Onesiforo; maana marra nyingi aliniburudisha, wala hakuutahayarikia mnyororo wangu;


Katika huyu nimeteswa kiasi cha kufungwa, kama mtenda mabaya; illakini neno la Mungu halifungwi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo