Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 21:31 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

31 Na walipokuwa wakitafuta njia ya kumwua, khabari zikamfikilia jemadari wa kikosi ya kwamba mji Yerusalemi umechafuka, mji mzima.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

31 Walikuwa tayari kumwua, lakini habari zilimfikia mkuu wa jeshi la Kiroma kuwa Yerusalemu yote ilikuwa imejaa ghasia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

31 Walikuwa tayari kumwua, lakini habari zilimfikia mkuu wa jeshi la Kiroma kuwa Yerusalemu yote ilikuwa imejaa ghasia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

31 Walikuwa tayari kumwua, lakini habari zilimfikia mkuu wa jeshi la Kiroma kuwa Yerusalemu yote ilikuwa imejaa ghasia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

31 Walipokuwa wakitaka kumuua, habari zikamfikia jemadari wa jeshi la askari Warumi kwamba mji wa Yerusalemu wote ulikuwa katika machafuko.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

31 Walipokuwa wakitaka kumuua, habari zikamfikia jemadari wa jeshi la askari wa Kirumi kwamba mji wa Yerusalemu wote ulikuwa katika machafuko.

Tazama sura Nakili




Matendo 21:31
19 Marejeleo ya Msalaba  

Wakanena, Sio wakati wa siku kuu, isije ikatokea ghasia katika watu.


Ndipo askari wa liwali wakamchukua Yesu ndani ya praitorio, wakamkusanyia kikosi kizima.


Kwa maana walisema, Sio wakati wa siku kuu, isije ikawa fitina katika watu.


Watawaharamisha masunagogi: naam, saa inakuja, atakapodhani killa mtu awauae kuwa amtolea Mungu ibada.


Bassi kile kikosi na yule jemadari na wale watumishi wa Wayahudi wakamkamata Yesu, wakanifunga,


PALIKUWA na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitaliano,


Na Wayahudi wasioamini wakaona wivu, wakajitwalia watu kadha wa kadha katika watu ovyo wasio na sifa njema wakakutanisha mkutano, wakafanya ghasia mjini, wakawaendea watu wa nyumba ya Yason wakataka kuwapeleka mbele ya watu wa mji;


Kwa maana tuna khatari ya kushtakiwa fitina kwa ajili ya mambo haya ya leo, ikiwa hakuna sababu ambayo kwa ajili yake tutaweza kujiudhuru kwa mkutano huu.


Wewe si vnle Mmisri ambae kabla ya siku hizi aliwafitinisha wale watu elfu nne, walioitwa Wauaji, akawaongoza jangwani?


Wakamsikiliza mpaka neno lile, wakapaaza sauti zao, wakisema, Mwondoe huyu katika inchi, kwa maana haifai aishi.


Paolo akamwita akida mmoja, akasema, Mchukue huyu kwa jemadari; maana ana neno la kumwarifu.


Bassi Feliki, alijiokwisha kusikia haya, aliwaakhirisha, kwa sababu alijua khabari za Njia ile kwa usahihi zaidi, akasema, Lusia jemadari, atakapotelemka nitakata maneno yenu.


Na tena alijaribu kuitia hekalu najis: tukamkamata: tukataka kumhukumu kwa sharia yetu.


Lakini Lusia jemadari akafika, akampokonya mikononi mwetu kwa nguvu, akawaamuru wale waliomshitaki waje kwako.


Hatta assubuhi Agrippa akaja pamoja na Bereniki kwa fakhari nyingi, wakapaingia mahali pa kusikia maneno, pamoja na maakida na watu wakuu wa mji: Festo akatoa amri Paolo aletwe.


Kwa sababu ya hayo Wayahudi wakanikamata ndani ya hekalu wakajaribu kuniua.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo