Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 21:3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

3 Na tulipoona Kupro tukaiacha upande wa kushoto: tukasafiri hatta Shami tukashuka Turo. Kwa maana huko ndiko marikebu yetu itakakoshusha shehena yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Baada ya kufika mahali ambapo tuliweza kuona Kupro, tulipitia upande wake wa kusini tukaelekea Siria. Tulitia nanga katika mji wa Tiro ambapo ile meli ilikuwa ipakuliwe shehena yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Baada ya kufika mahali ambapo tuliweza kuona Kupro, tulipitia upande wake wa kusini tukaelekea Siria. Tulitia nanga katika mji wa Tiro ambapo ile meli ilikuwa ipakuliwe shehena yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Baada ya kufika mahali ambapo tuliweza kuona Kupro, tulipitia upande wake wa kusini tukaelekea Siria. Tulitia nanga katika mji wa Tiro ambapo ile meli ilikuwa ipakuliwe shehena yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Tulipokiona kisiwa cha Kipro, tukakizunguka tukakiacha upande wetu wa kushoto, tukasafiri hadi Siria. Tukatia nanga katika bandari ya Tiro, ambapo meli yetu ilikuwa ipakue shehena yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Tulipokiona kisiwa cha Kipro, tukakizunguka tukakiacha upande wetu wa kushoto, tukasafiri mpaka Shamu, tukatia nanga katika bandari ya Tiro ambapo meli yetu ilikuwa ipakue shehena yake.

Tazama sura Nakili




Matendo 21:3
22 Marejeleo ya Msalaba  

Ole wako, Korazin! Ole wako, Bethsaida! Kwa maana kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Turo na Sidon, wangalitubu zamani kwa kuvaa gunia na majivu.


Khabari zake zikaenea katika Sham yote; wakamletea watu waliokuwa hawawezi, walioshikwa mi maradhi mbali mbali na mateso, nao wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya.


Ole wako, Korazin! Ole wako Bethsaida! kwa maana kama miujiza iliyofanyika kwenu, ingalifanyika katika Turo na Sodom, wangalitubu zamani, wakiketi katika nguo za kigunia na majivu.


orodha hii ndiyo ya kwanza iliyoandikwa wakati Kurenio alipotawala Sham.


Bassi wale waliotawanyika kwa sababu ya ile shidda iliyotukia kwa khabari ya Stefano, wakasafiri hatta Foiniki na Kupro na Antiokia, wasilikhubiri lile neno illa kwa Wayahudi peke yao.


Nae Herode aliwakasirikia sana watu wa Tʼuro na Sidon: wakamwendea kwa nia moja, na wakiislia kufanya urafiki na Blasto, mwenye kukitunza chumba cha mfalme cha kulalia, wakataka amani; kwa maana inchi yao ilipata riziki kwa inchi ya mfalme.


Bassi watu hao, wakiisha kupelekwa na Roho Mtakatifu wakatelemkia Selukia, na kutoka huko wakasafiri baharini hatta Kupro.


Wakaandika hivi kwa mikono yao, Mitume na wazee na ndugu, kwa ndugu zetu walioko Antiokia na Shami na Kilikia, walio wa mataifa, salamu.


Bassi palitokea maneno makali beina yao hatta wakatengana: Barnaba akamchukua Marko akatweka kwenda Kupro.


Akapita katika Shami na Kilikia akawatia moyo makanisa.


Paolo akazidi kukaa huko siku nyingi, kiisha akaagana na ndugu akatweka kwenda Shami; na Priskilla na Akula wakaenda pamoja nae, alipokwisha kunyoa kichwa chake katika Kenkrea; maana alikuwa ana nadhiri.


Baadhi ya wanafunzi wa Kaisaria wakafuatana na sisi, wakachukua na Mnason, mtu wa Kupro, mwanafunzi wa zamani ambae ndiye tutakaekaa kwake.


tukapata merikebu itakayovuka hatta Foiniki tukapanda tukatweka.


Hatta tulipomaliza safari yetu kutoka Troa tukafika Ptolemai, tukawasalimu ndugu tukakaa kwao siku moja.


Kutoka huko tukatweka, tukasafiri chini ya Kupro illi kuukinga upepo, kwa maana pepo zilikuwa za mbisho,


Na Yusuf, aliyeitwa na mitume Barnaba (tafsiri yake, Mwana wa faraja), Mlawi, asili yake ni mtu wa Kupro,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo