Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 21:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 Baadhi ya wanafunzi wa Kaisaria wakafuatana na sisi, wakachukua na Mnason, mtu wa Kupro, mwanafunzi wa zamani ambae ndiye tutakaekaa kwake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Baadhi ya wale wafuasi wa Kaisarea walikwenda pamoja nasi, wakatupeleka nyumbani kwa Mnasoni ambaye tulikuwa tunakwenda kukaa naye kwa muda. Mnasoni alikuwa mwenyeji wa Kupro na alikuwa amekuwa mwaamini kwa siku nyingi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Baadhi ya wale wafuasi wa Kaisarea walikwenda pamoja nasi, wakatupeleka nyumbani kwa Mnasoni ambaye tulikuwa tunakwenda kukaa naye kwa muda. Mnasoni alikuwa mwenyeji wa Kupro na alikuwa amekuwa mwaamini kwa siku nyingi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Baadhi ya wale wafuasi wa Kaisarea walikwenda pamoja nasi, wakatupeleka nyumbani kwa Mnasoni ambaye tulikuwa tunakwenda kukaa naye kwa muda. Mnasoni alikuwa mwenyeji wa Kupro na alikuwa amekuwa mwaamini kwa siku nyingi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Baadhi ya wanafunzi kutoka Kaisaria wakafuatana nasi na kutupeleka nyumbani mwa Mnasoni, ambaye tungekaa kwake. Yeye alikuwa mtu wa Kipro, mmoja wa wanafunzi wa zamani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Baadhi ya wanafunzi kutoka Kaisaria wakafuatana nasi na kutupeleka nyumbani kwa Mnasoni, ambaye tungekaa kwake. Yeye alikuwa mtu wa Kipro, mmoja wa wanafunzi wa zamani.

Tazama sura Nakili




Matendo 21:16
15 Marejeleo ya Msalaba  

Hatta siku ya pili yake wakaingia Kaisaria. Na Kornelio alikuwa akiwangojea, amekusanya jamaa zake na rafiki zake.


Akaamuru wabatizwe kwa Jina lake Yesu Kristo. Ndipo wakamsihi azidi kukaa siku kadha wa kadha.


Bassi wale waliotawanyika kwa sababu ya ile shidda iliyotukia kwa khabari ya Stefano, wakasafiri hatta Foiniki na Kupro na Antiokia, wasilikhubiri lile neno illa kwa Wayahudi peke yao.


Bassi palitokea maneno makali beina yao hatta wakatengana: Barnaba akamchukua Marko akatweka kwenda Kupro.


Na baada ya hoja nyingi Petro akasimama, akawaambia, Ndugu zangu, ninyi mnajua ya kuwa siku za kwanza Mungu alichagua miongoni mwetu mataifa walisikie neno la Injili kwa kinywa changu, na kuliamini.


Assubuhi yake sisi tulifuatana na Paolo tukatoka, tukafika Kaisaria, tukaingia nyumbani mwa Filipo, Mwinjilisti, aliyekuwa mmoja wa wale saba, tukakaa kwake.


Na Yusuf, aliyeitwa na mitume Barnaba (tafsiri yake, Mwana wa faraja), Mlawi, asili yake ni mtu wa Kupro,


Filipo akaonekana katika Azoto, na alipokuwa akipita akakhubiri Injili katika miji yote, hatta akafika Kaisaria.


Nisalimieni Androniko na Junia; jamaa zangu, waliofungwa pamoja nami, walio maarufu katika mitume; nao walikuwa katika Kristo kabla yangu.


illakini, kwa ajili ya upendo, nakusihi, kwa kuwa ni kama nilivyo, Paolo mzee, na sasa mfungwa wa. Yesu Krlsto pia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo