Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 20:35 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

35 Nimewapeni mfano katika mambo yote ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapaseni kuwasaidia wasio na nguvu, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni kheri kutoa kuliko kupokea.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

35 Nimekuwa nikiwapeni daima mfano kwamba kwa kufanya kazi mithili hiyo tunapaswa kuwasaidia walio dhaifu, tukikumbuka maneno ya Bwana Yesu mwenyewe: ‘Heri zaidi kutoa kuliko kupokea.’”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

35 Nimekuwa nikiwapeni daima mfano kwamba kwa kufanya kazi mithili hiyo tunapaswa kuwasaidia walio dhaifu, tukikumbuka maneno ya Bwana Yesu mwenyewe: ‘Heri zaidi kutoa kuliko kupokea.’”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

35 Nimekuwa nikiwapeni daima mfano kwamba kwa kufanya kazi mithili hiyo tunapaswa kuwasaidia walio dhaifu, tukikumbuka maneno ya Bwana Yesu mwenyewe: ‘Heri zaidi kutoa kuliko kupokea.’”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

35 Katika kila jambo nimewaonesha kwamba kwa njia hii ya kufanya kazi kwa bidii imetupasa kuwasaidia wadhaifu, mkikumbuka maneno ya Bwana Isa mwenyewe jinsi alivyosema, ‘Ni heri kutoa kuliko kupokea.’ ”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

35 Katika kila jambo nimewaonyesha kwamba kwa njia hii ya kufanya kazi kwa bidii imetupasa kuwasaidia wadhaifu, mkikumbuka maneno ya Bwana Isa mwenyewe jinsi alivyosema, ‘Ni heri kutoa kuliko kupokea.’ ”

Tazama sura Nakili




Matendo 20:35
28 Marejeleo ya Msalaba  

Ponyeni wagonjwa, takaseni wenye ukoma, fufueni wafu, fukuzeni pepo; mmepata burre, toeni burre.


ya kuwa sikuficha neno lo lote liwezaio kuwafaeni, bali naliwaonyesha na kuwafundisha kwa wazi na nyumba kwa nyumba,


Kwa maana sikujiepusha na kuwakhubirini khabari ya shauri lote la Mungu.


Ninyi wenyewe mnajua ya kuwa mikono hii imetumika kwa mahitaji yangu na yao walio pamoja nami.


Alipokwisha kunena haya akapiga magoti, akaomba pamoja nao wote.


BASSI imetupasa sisi tulio na nguvu kuuchukua udhaifu wao wasio na nguvu, wala haitupasi kujipendeza nafsi zetu.


Ikiwa wengine wanashiriki uwezo huu juu yenu, sisi si zaidi? Lakini hatukuutumia uwezo huu; bali twayavumilia mambo yote tusije tukaizuia Injili ya Kristo.


Lakini nifanyalo nitalifunya, illi niwapinge watafutao nafasi wasipate nafasi; illi katika neno hilo wajisifulo waonekane kuwa kama sisi.


Nami nilipokuwa pamoja nanyi na kuhitaji sikumlemea mtu. Maana ndugu walipokuja kutoka Makedonia walinipa kadiri ya mahitaji yangu; na katika mambo yote nalijilinda nafsi yangu nisiwalemee hatta kidogo; tena nitajilinda.


Maana ni kitu gani mlichopungukiwa kuliko makanisa mengine, illa kwa kuwa mimi sikuwalemea. Mnisamehe udhalimu huo.


Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yetu, alipokuwa tajiri, illi ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.


Mwibaji asiibe tena; bali afadhali afanye juhudi, akitenda kazi iliyo njema kwa mikono yake mwenyewe, apafe kuwa na kitu cha kumgawia mhitaji.


tena mjitahidi kutulia, na kutenda shughuli zenu na kufanya kazi kwa mikono yenu wenyewe kama tulivyowaagiza;


Twawasihi, ndugu, waonyeni wale wasiokaa kwa taratihu, watieni moyo walio dhaifu, watieni nguvu wanyonge, vumilieni na watu wote.


Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana na watu; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu.


Wakumbukeni waliofungwa kana kwamba mmefungwa pamoja nao; nao wanaodhulumiwa, kwa kuwa nanyi m katika mwili.


Kwa maana, kwa ajili ya Jina hilo, walitoka, wasipokee kilu kwa mataifa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo