Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 20:32 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

32 Bassi, sasa ndugu, nawawekeni katika mikono ya Mungu, na kwa neno la neema yake, kwake yeye awezae kuwajengeni na kuwapeni urithi pamoja nao wote waliotakasika.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

32 “Na sasa basi, ninawaweka nyinyi chini ya ulinzi wa Mungu na ujumbe wa neema yake. Yeye anao uwezo wa kuwajenga na kuwawezesha mzipate zile baraka alizowawekea watu wake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

32 “Na sasa basi, ninawaweka nyinyi chini ya ulinzi wa Mungu na ujumbe wa neema yake. Yeye anao uwezo wa kuwajenga na kuwawezesha mzipate zile baraka alizowawekea watu wake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

32 “Na sasa basi, ninawaweka nyinyi chini ya ulinzi wa Mungu na ujumbe wa neema yake. Yeye anao uwezo wa kuwajenga na kuwawezesha mzipate zile baraka alizowawekea watu wake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

32 “Sasa nawakabidhi kwa Mungu na kwa neno la neema yake, linaloweza kuwajenga na kuwapa ninyi urithi miongoni mwa wote ambao wametakaswa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

32 “Sasa nawakabidhi kwa Mwenyezi Mungu na kwa neno la neema yake, linaloweza kuwajenga na kuwapa ninyi urithi miongoni mwa wote ambao wametakaswa.

Tazama sura Nakili




Matendo 20:32
37 Marejeleo ya Msalaba  

Hatta alipokuwa akitoka kwenda njiani mtu mmoja akaja mbio, akampigia magoti, akamwuliza, Mwalimu mwema, nifanyeni nipate kuurithi uzima wa milele?


Ninyi mmekwisba kuwa safi kwa sababu ya neno nililowaambia.


Uwatakase kwa kweli; neno lako ndio kweli.


Nae, alipokwisha kufika na kuiona neema ya Mungu akafurahi, akawasihi wote waambatane na Bwana kwa kusudi la moyo.


Na walipokwisha kuchagua wazee katika killa mji, na kuomba pamoja na kufunga, wakawaweka kafika mikono ya Bwana waliyemwamini.


Na kutoka huko wakasafiri baharini kwenda Antiokia. Huko ndiko walikoombewa neema ya Mungu kwa ile kazi waliyokwisha kuitimiza.


Bassi wakakaa huko wakati mwingi, wakinena kwa uthabiti katika Bwana, aliyelishuhudia neno la neema yake, akiwajalia ishara na maajabu yatendeke kwa mikono yao.


Paolo akamchagua Sila akaondoka, akiombewa na wale ndugu, apewe neema ya Mungu.


Lakini siyahesabu maisha yaugu kuwa kitu cha thamani kwangu kama kuumaliza mwendo wangu na khuduma ile niliyopokea kwa Bwana Yesu, kuishuhudia Injili ya neema ya Mungu.


uwafumhue macho yao, waiache giza na kuielekea nuru, na waziache nguvu za Shetani na kumwelekea Mungu, na wapate masamaha ya dhambi zao, na urithi miongoni mwao waliotakaswa kwa imani iliyo kwangu.


Bassi makanisa wakapata raha katika Yahudi yote na Galilaya na Samaria, wakajengewa, wakiendelea katika kicho cha Bwana, na faraja ya Roho Mtakatifu.


kama tu watoto, bassi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja nae illi tutukuzwe pamoja nae.


kwa kanisa la Mungu lililo katika Korintho, lililotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu pamoja na wote wanaoliitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo killa mahali, Bwana wao na wetu:


wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyangʼanyi.


Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hizi; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa kuwa na haki katika jina la Bwana Yesu na katika Roho ya Mungu wetu.


Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike. Waasharati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wa kike, wala wafira,


aliye arabuni ya urithi wetu, hatta ukombozi wa milki yake Mungu, kwa sifa ya utukufu wake.


macho ya akili zenu yakitiwa nuru, mjue tumaini la wito wake jinsi lilivyo, na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo,


kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, kazi ya khuduma itendeke, mwili wa Kristo ujengwe;


katika yeye mwili wote ukiungamanishwa na kushikanishwa, kwa msaada wa killa kiungo, kwa kadiri ya kazi ya killa sehemu moja moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo.


Maana neno hili mnalijua kwa kulifaliamu, kwamba hapana asharati, wala mchafu, wala mtu wa tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu.


mkimshukuru Baba, aliyetustahilisha kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu katika nuru;


mmetia mizizi, na kujengwa katika yeye: mmefanywa imara kwa imani, kaina mlivyofundishwa, mkizidi kutoa shukrani.


mkijua ya kuwa mtapokea kwa Bwana njira wa urithi; kwa kuwa mnamtumikia Bwana Kristo.


Maana kwa toleo moja amewakamilisha hatta milele wanaotakaswa.


Msichukuliwe na mafundisho ya namna nyingine nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa neema, wala si kwa vyakula, ambavyo wao waliokwenda navyo bawakupata faida.


Maana yeye atakasae nao wanaotakaswa wote pia watoka kwa mmoja. Kwa ajili hii haoni haya kuwaita ndugu zake;


Na kwa sababu hii yu mjumbe wa agauo jipya, illi, mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa ya katika agano la kwanza, walioitiwa waipokee ahadi ya urithi wa milele.


YUDA, mtumwa wa Yesu Kristo, ndugu wa Yakobo, kwao waliopendwa katika Mungu Baba, na kuhifadhiwa kwa ajili ya Yesu Kristo baada ya kuitwa;


Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imaui yenu iliyo takatifu, na kuomba katika Roho Mtakatifu,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo