Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 20:31 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

31 Kwa biyo kesheni, mkikumbuka kama miaka mitatu, usiku na mchana, sikuacha kumwonya killa mtu kwa machozi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

31 Kwa hiyo, muwe macho mkikumbuka kwamba kwa muda wa miaka mitatu, usiku na mchana, sikuchoka kumwonya kila mmoja wenu kwa machozi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

31 Kwa hiyo, muwe macho mkikumbuka kwamba kwa muda wa miaka mitatu, usiku na mchana, sikuchoka kumwonya kila mmoja wenu kwa machozi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

31 Kwa hiyo, muwe macho mkikumbuka kwamba kwa muda wa miaka mitatu, usiku na mchana, sikuchoka kumwonya kila mmoja wenu kwa machozi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

31 Hivyo jilindeni! Kumbukeni kwamba kwa miaka mitatu sikuacha kamwe kuwaonya kila mmoja kwa machozi usiku na mchana.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

31 Hivyo jilindeni! Kumbukeni kwamba kwa miaka mitatu sikuacha kamwe kuwaonya kila mmoja kwa machozi usiku na mchana.

Tazama sura Nakili




Matendo 20:31
22 Marejeleo ya Msalaba  

lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya nganu, akaenda zake.


Hatta akiona wengi miongoni mwa Mafarisayo na Masadukayo wakiujia ubatizo wake, akawaambia, Uzao wa nyoka, nani aliyewaonya mkimbie ghadhabu ijayo?


Kwa hiyo kesheni killa wakati, mkiomba mpate kuhesabiwa kuwa mmestahili kuponea haya yote yatakayokuwa, na kusimama mahali penu mbele ya Mwana wa Adamu.


Mambo haya yakaendelea kwa muda wa miaka miwili, hatta wote waliokaa Asia wakalisikia neno la Bwana, Wayahudi kwa Wayunani.


Akaingia ndani ya sunagogi, akanena kwa ujasiri, akihujiana na watu kwa muda wa miezi mitatu, na kuwavuta waamini mambo ya ufalme wa Mungu.


Akapanda juu tena, akamega mkate, akala, akazidi kuongea nao hatta alfajiri, ndipo akaenda zake.


nikimtumikia Bwana kwa unyenyekevu wote, na machozi, na majaribu yaliyonipata kwa hila za Wayahudi;


Hatta siku ya kwanza ya juma, wanafunzi walipokusanyika illi kumega mkate, Paolo akawakhutubu, akaazimu kusafiri siku ya pili yake, akafuliza maneno yake mpaka nsiku wa manane.


Baada ya miaka mingi nalifika niwaletee watu wa taifa langu sadaka na matoleo.


Siyaandiki haya illi kuwatahayarisha, hali kuwaonya kama watoto niwapendao. Maana ijapokuwa mna waalimu elfu katika Kristo, illakini hamna baba wengi.


Maana wengi huenenda, nimewaambieni marra nyingi khabari zao, na hatta sasa nawaambieni kwa machozi, kuwa ni adui za msalaba wa Kristo;


ambae sisi tunakhubiri khabari zake, tukimwonya killa mtu, na tukimfundisha killa mtu katika hekima yote, tupate kumleta killa mtu mtimilifu katika Kristo Yesu;


Twawasihi, ndugu, waonyeni wale wasiokaa kwa taratihu, watieni moyo walio dhaifu, watieni nguvu wanyonge, vumilieni na watu wote.


Hamkumbuki ya kuwa wakati nilipokuwa pamoja nanyi naliwaambieni hayo?


wala hatukula chakula kwa mtu ye yote burre, bali kwa taabu na masumbufu, mchana na usiku, tulitenda kazi, illi tusimlemee mtu kwenu;


Bali wewe erevuka katika yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mwinjilisti, timiliza khuduma yako.


Watiini walio na mamlaka juu yenu, na kujinyenyekea kwao; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, illi wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi.


Tazama, naja kama mwizi. Yu kheri akeshae, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi wakaone aibu yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo