Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 20:3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

3 Alipokwisha kukaa huko miezi mitatu, Wayahudi wakamfanyyia vitimbi, alipotaka kwenda Sham kwa njia ya bahari: bassi akaazimu kurejea kwa ujia ya Makedonia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 ambako alikaa kwa miezi mitatu. Alipokuwa anajitayarisha kwenda Siria, aligundua kwamba Wayahudi walikuwa wanamfanyia mpango mbaya; hivyo aliamua kurudi kwa kupitia Makedonia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 ambako alikaa kwa miezi mitatu. Alipokuwa anajitayarisha kwenda Siria, aligundua kwamba Wayahudi walikuwa wanamfanyia mpango mbaya; hivyo aliamua kurudi kwa kupitia Makedonia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 ambako alikaa kwa miezi mitatu. Alipokuwa anajitayarisha kwenda Siria, aligundua kwamba Wayahudi walikuwa wanamfanyia mpango mbaya; hivyo aliamua kurudi kwa kupitia Makedonia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 ambako alikaa kwa muda wa miezi mitatu. Kwa sababu baadhi ya Wayahudi walikuwa wamepanga njama dhidi yake alipokuwa karibu kusafiri kwa meli kwenda Siria, aliamua kurudi kupitia Makedonia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 ambako alikaa kwa muda wa miezi mitatu. Alipokuwa anakaribia kuanza safari kwa njia ya bahari kwenda Shamu, kwa sababu Wayahudi walikuwa wamefanya shauri baya dhidi yake, aliamua kurudi kupitia njia ya Makedonia.

Tazama sura Nakili




Matendo 20:3
19 Marejeleo ya Msalaba  

Khabari zake zikaenea katika Sham yote; wakamletea watu waliokuwa hawawezi, walioshikwa mi maradhi mbali mbali na mateso, nao wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya.


Siku ya pili tukafika Neapoli na kutoka hapo tukafika Filippi, mji wa Makedonia, mji ulio mkuu katika wilaya ile, nayo ni Kolonia ya Kirumi; tukawa katika mji huu, tukikaa siku kadha wa kadha.


Paolo akatokewa na maono usiku; alimwona mtu wa Makedonia amesimama, akimsihi akimwambia, Vuka uje Makedonia utusaidie.


Paolo akazidi kukaa huko siku nyingi, kiisha akaagana na ndugu akatweka kwenda Shami; na Priskilla na Akula wakaenda pamoja nae, alipokwisha kunyoa kichwa chake katika Kenkrea; maana alikuwa ana nadhiri.


Mambo hayo yalipokwisha kumalizika, Paolo akaazimu rohoni mwake kupita kati ya Makedonia na Akaia aende Yerusalemi, akisema, Baada ya kuwako huko, yanipasa kuuona na Rumi.


KISHINDO kile kilipokoma, Paolo akawaita wanafunzi akaagana nao, akaondoka aende zake hatta Makedonia.


nikimtumikia Bwana kwa unyenyekevu wote, na machozi, na majaribu yaliyonipata kwa hila za Wayahudi;


Na, akiisha kupita pande zile na kuwafariji kwa maneno mengi, akafika Uyunani.


Na tulipoona Kupro tukaiacha upande wa kushoto: tukasafiri hatta Shami tukashuka Turo. Kwa maana huko ndiko marikebu yetu itakakoshusha shehena yake.


na kumwomba awafadhili, na kutoa amri aletwe Yerusalemi, wapate kumwotea na kumwua njiani.


Na nikiwa na timiaini hilo nalitaka kwenda kwenu hapo kwanza, illi mpate karama ya pili;


kwa kusafiri marra nyingi; khatari za mito; khatari za wanyangʼanyi; khatari kwa jamaa; khatari kwa mataifa; khatari za mijini; khatari za jangwani; khatari za baharini; khatari kwa ndugu za uwongo;


Kwa maana hatta tulipokuwa tumelikia Makedonia miili yetu haikupata nafuu; bali tuliteswa kote kote; nje palikuwa na vita, ndani khofu.


Khalafu nalikwenda pande za Sham na Kilikia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo