Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 20:28 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

28 Jiangalieni nafsi zenu, na kundi lote, ambalo Roho Mtakatifu aliwakabidhi mlisimamie, kanisa lake Mungu, alilojipatia kwa damu yake mwenyewe.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

28 Jihadharini wenyewe; lilindeni lile kundi ambalo Roho Mtakatifu amewaweka nyinyi muwe walezi wake. Lichungeni kanisa la Mungu ambalo amejipatia kwa damu ya Mwanae.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

28 Jihadharini wenyewe; lilindeni lile kundi ambalo Roho Mtakatifu amewaweka nyinyi muwe walezi wake. Lichungeni kanisa la Mungu ambalo amejipatia kwa damu ya Mwanae.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

28 Jihadharini wenyewe; lilindeni lile kundi ambalo Roho Mtakatifu amewaweka nyinyi muwe walezi wake. Lichungeni kanisa la Mungu ambalo amejipatia kwa damu ya Mwanae.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

28 Jilindeni nafsi zenu na mlilinde lile kundi lote ambalo Roho wa Mungu amewaweka ninyi kuwa waangalizi wake. Chungeni jumuiya ya waumini ya Mungu, aliowanunua kwa damu yake mwenyewe.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

28 Jilindeni nafsi zenu na mlilinde lile kundi lote ambalo Roho wa Mwenyezi Mungu amewaweka ninyi kuwa waangalizi wake. Lichungeni kundi la waumini lake Mungu alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.

Tazama sura Nakili




Matendo 20:28
61 Marejeleo ya Msalaba  

Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na jun ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; na milango ya kuzimu haitalishinda.


Na wewe Bethlehemu wa inchi ya Yuda, Huwi mdogo kamwe katika majumbe ya Yuda: Kwa kuwa kwako atatoka liwali Atakaewachunga watu wangu Israeli.


Nanyi jihadharini nafsi zenu; maana watawapelekeni maharazani: na katika masunagogi mtapigwa: na mtachukuliwa mbele za maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao.


Msiogope, enyi kundi dogo, kwa kuwa Baba yenu ameona vyema kuwapeni ufalme.


Bassi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi na ulevi, na masumbufu ya maisha haya,


Bassi hawa walipokuwa wakimkhudumia Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Niwekeeni Barnaba na Saul kwa kazi ile niliyowaitia.


Na walipokwisha kuchagua wazee katika killa mji, na kuomba pamoja na kufunga, wakawaweka kafika mikono ya Bwana waliyemwamini.


Toka Mileto Faolo akatuma watu kwenda hatta Efeso, akawaita wazee wa Kanisa.


Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa za mwitu wakali watakuja kwenu, wasiliachie kundi:


Salimianeni kwa busu takatifu. Makanisa yote ya Kristo yawasalimu.


kwa kanisa la Mungu lililo katika Korintho, lililotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu pamoja na wote wanaoliitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo killa mahali, Bwana wao na wetu:


Msiwakoseshe Wayahudi wala Wayunaui wala Kanisa la Mungu:


Je! hamna nyumba za kulia na kunywea? Au mnalidharau Kanisa la Mungu, na kuwatahayarisha wasio na kitu? Niwaambieni? niwasifu kwa haya? Siwasifu.


Maana mimi mdogo katika mitume, nisiyestahili kutajwa mtume, kwa sababu naliliudhi Kanisa la Mungu.


Maana mlinunuliwa kwa thamani. Kwa kuwa ni hivyo, mtukuzeni Mungu kwa mwili wenu, na kwa roho yenu, ambayo ni mali ya Mungu.


Maana mmesikia khabari za mwenendo wangu zamani katika dini ya Kiyahudi, kwamba naliliudhi kanisa la Mungu kupita kiasi nikaliharibu,


aliye arabuni ya urithi wetu, hatta ukombozi wa milki yake Mungu, kwa sifa ya utukufu wake.


Katika yeye tuna ukombozi kwa damu yake, masamaha ya dhambi, kwa wingi wa neema yake;


Na yeye aliwatoa wengine kuwa mitume; na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti, na wengine kuwa wachungaji, na waalimu,


PAOLO na Timotheo, watumwa wa Yesu Kristo, kwa watakatifu wote katika Kristo Yesu, walio katika Filipi, pamoja na maaskofu na wakhudumu;


amliae katika yeye tuna nkombozi kwa damu yake, masamaha ya dhambi,


Mwambieni Arkippo, Iangalie sana khuduma ile uliyopewa katika Bwana, illi uitimize.


AMINI neno hili, Mtu akitaka uaskofu, atamani kazi nzuri.


Bassi imempasa askofu kuwa mtu asiyelaumiwa, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, mfundishaji;


(mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje kanisa la Mungu?)


Usiache kuitumia ile karama iliyo udani yako uliyopewa wewe kwa unabii, na kwa kuwekewa mikono ya wazee.


Jitunze nafsi yako, na yale mafundisho. Ukadumu katika hayo; maana kwa kufanya hivi utajiokoa nafsi yako nao wakusikiao.


Wazee watawalao vema wapewe heshima mardufu, khassa wao wajitaabishao kwa kukhutubu na kufundisha.


Maana imempasa askofu awe mtu asioshitakiwa neno, kwa kuwa ni wakili wa Mungu; asiwe mtu wa kujipendeza nafsi yake, asiwe mwepesi wa hasira, asiwe mzoelea mvinyo, asiwe mpigaji, asiwe mpenda mapato ya aibu,


aliyejitoa nafsi yake kwa ajili yetu, illi atuokoe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake, walio na juhudi kwa matendo mema.


mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua watu wengi, wakatiwe najis kwa hilo.


Watiini walio na mamlaka juu yenu, na kujinyenyekea kwao; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, illi wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi.


Kwa maana mlikuwa kama kondoo wanaopotea; lakini sasa mmemrudia Mchunga na Askofu wa roho zenu.


Bali ninyi m mzao mteule, ukubani wa kifaume, taifa takatifu, watu wa milki, mpate kutangaza fadhili zake aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;


bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu Kristo, Mwana wake, yatusafisha dhambi zote.


Nao waimba uimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulicbinjwa


Tufuate:

Matangazo


Matangazo