Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 20:24 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

24 Lakini siyahesabu maisha yaugu kuwa kitu cha thamani kwangu kama kuumaliza mwendo wangu na khuduma ile niliyopokea kwa Bwana Yesu, kuishuhudia Injili ya neema ya Mungu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 Lakini, siuthamini uhai wangu kuwa kitu sana kwangu mradi tu nikamilishe ule utume wangu na ile kazi aliyonipa Bwana Yesu niifanye, yaani nishuhudie Habari Njema ya neema ya Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 Lakini, siuthamini uhai wangu kuwa kitu sana kwangu mradi tu nikamilishe ule utume wangu na ile kazi aliyonipa Bwana Yesu niifanye, yaani nishuhudie Habari Njema ya neema ya Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 Lakini, siuthamini uhai wangu kuwa kitu sana kwangu mradi tu nikamilishe ule utume wangu na ile kazi aliyonipa Bwana Yesu niifanye, yaani nishuhudie Habari Njema ya neema ya Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 Lakini siyahesabu maisha yangu kuwa ya thamani kwangu, kama kuyamaliza mashindano na kukamilisha ile kazi Bwana Isa aliyonipa, yaani kazi ya kuishuhudia Injili ya neema ya Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 Lakini siyahesabu maisha yangu kuwa ya thamani kwangu, kama kuyamaliza mashindano na kukamilisha ile kazi Bwana Isa aliyonipa, yaani, kazi ya kuishuhudia Injili ya neema ya Mungu.

Tazama sura Nakili




Matendo 20:24
59 Marejeleo ya Msalaba  

maana nina ndugu watano; awashuhudie, wasije nao mahali hapa pa adhabu.


Na ninyi pia mnashunudu, kwa kuwa tangu mwanzo mmekuwa pamoja nami.


Mimi nimekutukuza duniani. Kazi ile uliyonipa niifanye nimeimaliza.


akapata sehemu ya khuduma hii.


Nae, alipokwisha kufika na kuiona neema ya Mungu akafurahi, akawasihi wote waambatane na Bwana kwa kusudi la moyo.


Nae Yohana alipokuwa akimaliza mwendo wake alinena, Mwanidhani mimi kuwa nani? Mimi siye. Lakini, angalieni, anakuja mmoja nyuma yangu ambae mimi sistahili kumlegezea viatu vya miguu yake.


Bassi wakakaa huko wakati mwingi, wakinena kwa uthabiti katika Bwana, aliyelishuhudia neno la neema yake, akiwajalia ishara na maajabu yatendeke kwa mikono yao.


Na baada ya hoja nyingi Petro akasimama, akawaambia, Ndugu zangu, ninyi mnajua ya kuwa siku za kwanza Mungu alichagua miongoni mwetu mataifa walisikie neno la Injili kwa kinywa changu, na kuliamini.


Hatta Sila na Timotheo walipotelemka kutoka Makedonia, Paolo akashurutishwa rohoni mwake, akiwashuhudia Wayahudi ya kwamba Yesu ni Kristo.


nikiwashuhudia Wayahudi na Wayunani toba iliyo kwa Mungu, na imani iliyo kwa Bwana wetu Yesu Kristo.


illa ya kuwa Roho Mtakatifu mji kwa mji hunishuhudia akisema, ya kwamba vifungo na mateso yaningoja.


Bassi, sasa ndugu, nawawekeni katika mikono ya Mungu, na kwa neno la neema yake, kwake yeye awezae kuwajengeni na kuwapeni urithi pamoja nao wote waliotakasika.


Paolo akajibu, Mnafanyaje, kulia na kunivnnja moyo? kwa maana mimi, licha ya kufungwa tu, ni tayari hatta kuuawa katika Yerusalemi kwa ajili ya jina lake Bwana Yesu.


Nae akaniambia, Enenda zako; kwa kuwa mimi nitakutuma mbali kwa watu wa mataifa.


Lakini Bwana akamwambia, Shika njia; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli.


Lakini ikiwa ni kwa neema yake, haiwi kwa matendo tena, au hapo neema isingekuwa neema; na ikiwa ni kwa matendo, haiwi neema tena, au hapo matendo yasingekuwa matendo.


Lakini kwa mtu afanyae kazi ujira wake hauhesabiwi kuwa neema bali kuwa deni.


Bassi, ndugu wapendwa, mwe imara, msiotikisika, mkizidi sana kutenda kazi ya Bwana siku zote, kwa kuwa taabu yenu siyo burre katika Bwana.


Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na maumivu, na dhiiki, na adha, na shidda, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo ua nguvu.


KWA sababu hiyo, kwa kuwa tuna khuduma hii, kwa jinsi tulivyorehemiwa, hatulegei;


Bassi hapo mauti hufanya kazi yake ndani yetu, hali nzima ndani yenu.


Lakini tuna moyo mkuu; na tunaona vema zaidi kutoka katika mwili na kukaa pamoja na Bwana.


Nina ujasiri mwingi kwemi; kujisifu kwangu kwa ajili yenu ni kwingi. Nimejawa na faraja, katika mateso yetu yote nimejaa furaha ya kupita kiasi.


PAOLO, mtume (si mtume wa wana Adamu, wala hakutumwa na mwana Adamu, bali na Yesu Kristo, na Mungu Baba aliyemfufua),


illi usifiwe utukufu wa neema yake, aliyotukarimu katika mpendwa wake:


Bassi naomba, msikate tamaa kwa sababu ya mateso yangu kwa ajili yenu, yaliyo utukufu kwenu.


Naam, hatta nikimiminwa juu ya dhabihu na khuduma ya imani yenu, nafurahi; tena nafurahi pamoja nanyi nyote.


Maana kwa ajili ya kazi ya Kristo alikaribia kufa, asiutunze uhayi wake; illi kusudi ayatimize yaliyopungua katika khuduma yenu kwangu.


Sasa nayafurahia mateso niliyo nayo kwa ajili yenu; tena natimiliza yale yaliyopungua ya mateso ya Kristo katika mwili wangu, kwa ajili ya mwili wake, yaani, kanisa lake,


bali tukiisha kuteswa kwanza na kutendwa jeuri, kama mjuavyo, katika Filippi, twalithubutu katika Mungu kuinena Injili ya Mungu kwenu, kwa kuishindania sana.


mtu asifadhaishwe na mateso haya: maana ninyi wenyewe mnajua ya kuwa twawekewa haya.


Kwa sababu hiyo nimepata mateso haya, wala sitahayariki: maana namjua yeye niliyemwamini, na kusadiki kwamba aweza kukilinda kile nilichakiweka amana kwake hatta siku ile.


tena adha zangu na mateso yaliyonipata katika Antiokia, katika Ikonio, na katika Lustra; killa namna ya adha niliyoistahimili: nae Bwana akaniokoa katika yote.


Lakini Bwana alisimama pamoja nami akanitia nguvu, illi kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu, mataifa wrote wakasikie; nikaokolewa katika kanwa la simba.


akalifunua neno lake kwa nyakati zake katika ule ujumbe nilioaminiwa mimi kwa amri ya Mwokozi wetu, Mungu:


Maana neema ya Mungu iwaokoayo wana Adamu wote imeonekana;


Maana mliwaonea huruma wale waliokuwa katika mafungo, mkakubali kwa furaba kunyangʼauywa mali zenu, mkijua nafsini mwenu kwamba mna mali mbinguni iliyo njema zaidi, idumnyo.


Kwa mkono wa Silwano, ndugu mwaminifu kama nionavyo, nimewaandikieni kwa maneno machache, nikionya na kushuhudia ya kuwa hii ndiyo neema ya kweli va Mungu. Simameni imara katika hiyo.


Hivi tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliweka maisha yake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuweka maisha yetu kwa ajili ya ndugu.


Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; wala hawakupenda maisha yao hatta wakati wa kufa.


Wakapewa killa mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hatta itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao watakaouawa vile vile kama wao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo