Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 2:47 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

47 wakimsifu Mungu, na kuwapendeza wutu wote. Bwana akalizidisha kanisa killa siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

47 Walimtukuza Mungu, wakapendwa na watu wote. Kila siku Bwana aliwaongezea idadi ya watu waliokuwa wakiokolewa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

47 Walimtukuza Mungu, wakapendwa na watu wote. Kila siku Bwana aliwaongezea idadi ya watu waliokuwa wakiokolewa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

47 Walimtukuza Mungu, wakapendwa na watu wote. Kila siku Bwana aliwaongezea idadi ya watu waliokuwa wakiokolewa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

47 wakimsifu Mungu na kuwapendeza watu wote. Kila siku Bwana akaliongeza kundi la waumini wa Isa wale waliokuwa wakiokolewa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

47 wakimsifu Mwenyezi Mungu na kuwapendeza watu wote. Kila siku Bwana Mwenyezi akawaongeza waumini wale waliokuwa wakiokolewa.

Tazama sura Nakili




Matendo 2:47
25 Marejeleo ya Msalaba  

nao bawakuona la kutenda; maana watu wote waliambatana nae, wakimsikiliza.


Yesu akazidi kuendelea katika hekima, na kimo, na neema kwa Mungu na kwa watu.


Mkono wa Bwana ukawa pamoja nao: watu wengi wakaamini, wakamwelekea Bwana.


Maana alikuwa mtu mwema, amejaa Roho Mtakatifu na imani: watu wengi wakajitia upande wa Bwana.


Mataifa waliposikia hayo wakafurahi, wakalitukuza neno la Bwana, nao waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini.


IKAWA huko Ikonio wakaingia pamoja katika sunagogi ia Wayahudi, wakanena; hatta jamaa kubwa ya Wayahudi na ya Wayunani wakaamini.


Hatta walipokwisha kuikhubiri Injili katika niji ule, na kupata wanafunzi wengi, wakarejea hatta Lustra na Ikonio na Antiokia,


Makanisa yakatiwa nguvu kwa imani, hesabu yao ikaongezeka killa siku.


Wafu wengi wakaamini miongoni mwao, nao wanawake wa Kiyunani wenye cheo, na wanaume si wachache.


Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na watoto wenu, na watu wote walio mbali, na wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu.


Nao waliolipokea neno lake kwa furaha wakabatizwa: na siku ile wakazidishiwa watu wapata elfu tatu.


Nao walipokwisha kuwaogofya tena wakawafungua, wasione njia ya kuwaadhibu, kwa sababu ya watu: kwa kuwa watu wote walikuwa wakimtukuza Mungu kwa hayo yaliyotendeka:


Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa uguvu nyingi. Neema nyingi ikawa juu yao wote.


Lakini wengi katika hao waliosikia lile neno waliamini: na hesabu ya watu ilikuwa kama elfu tano.


HATTA siku ziie wanafunzi walipokuwa wakiongezeka hesabu yao, palikuwa na manungʼuniko ya Wahelenisti juu ya Waebrania kwa sababu wajane wao walisahauliwa katika khuduma ya killa siku.


Nenu la Mungu likaenea: hesahu ya wanafunzi ikazidi sana katika Yerusalemi: jamii kubwa la makuhani wakaitii Imani.


Bassi makanisa wakapata raha katika Yahudi yote na Galilaya na Samaria, wakajengewa, wakiendelea katika kicho cha Bwana, na faraja ya Roho Mtakatifu.


Marra akaondoka. Na watu wote waliokaa Ludda na Saron wakamwona, wakamgeukia Bwana.


Kwa kuwa yeye amtumikiae Kristo katika mambo haya humpendeza Mungu, tena hukubaliwa na wana Adamu.


Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hawa akawatukuza.


Isaya nae atoa santi yake juu ya Israeli, Hesabu ya wana wa Israeli, ijapokuwa kama mchanga wa bahari, ni mabaki yao tu watakaookolewa.


Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo