Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 2:43 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

43 Killa mtu akaingiwa na khofu: ajabu nyingi na ishara zikafanyika kwa ujumbe wa mitume.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

43 Miujiza na maajabu mengi yalifanyika kwa njia ya mitume hata kila mtu akajawa na hofu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

43 Miujiza na maajabu mengi yalifanyika kwa njia ya mitume hata kila mtu akajawa na hofu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

43 Miujiza na maajabu mengi yalifanyika kwa njia ya mitume hata kila mtu akajawa na hofu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

43 Kila mtu akaingiwa na hofu ya Mungu, nayo miujiza mingi na ishara zikafanywa na mitume.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

43 Kila mtu akaingiwa na hofu ya Mungu, nayo miujiza mingi na ishara zikafanywa na mitume.

Tazama sura Nakili




Matendo 2:43
15 Marejeleo ya Msalaba  

Na ishara hizi zitafuatana nao waaminio; Kwa jina langu watafukuza pepo; watasema kwa ndimi mpya;


Khofu ikawashika wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Nabii mkuu ametokea kwetu: na Mungu amewajilia watu wake.


Na watu wote wa inchi ya Wagadarene iliyo kando kando wakamwomba aondoke kwao, kwa sababu walishikwa na khofu nyingi; bassi akakiingia chombo akarudi.


Amin, amin, nawaambieni, Aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi na yeye atazifanya; atafanya na kubwa kuliko hizi, kwa kuwa nashika njia kwenda kwa Baba.


Enyi waume wa Israeli, sikieni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua;


Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa uguvu nyingi. Neema nyingi ikawa juu yao wote.


Anania aliposikia maneno haya akaanguka, akafa. Khofu nyiugi ikawapata watu wote walioyasikia haya.


Petro akamwambia, Ainea, Yesu Kristo akuponya: ondoka, ukatandike kitanda chako.


Petro akawatoa wote, akapiga magoti, akaomba, akaielekea mayiti, akanena, Tabitha, ondoka. Nae akafumbua macho yake, na alipomwona Petro akajiinua, akaketi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo