Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 2:42 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

42 Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

42 Hawa wote waliendelea kujifunza kutoka kwa mitume, kuishi pamoja kindugu, kumega mkate na kusali.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

42 Hawa wote waliendelea kujifunza kutoka kwa mitume, kuishi pamoja kindugu, kumega mkate na kusali.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

42 Hawa wote waliendelea kujifunza kutoka kwa mitume, kuishi pamoja kindugu, kumega mkate na kusali.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

42 Nao wakadumu katika mafundisho ya mitume, katika ushirika, katika kumega mkate na katika kusali.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

42 Nao wakawa wanadumu katika mafundisho ya mitume, katika ushirika, katika kumega mkate na katika kusali.

Tazama sura Nakili




Matendo 2:42
35 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa, akiketi pamoja nao, akautwaa mkate, akaubariki, akaumega, akawagawia.


Nao wakawahadithia yale ya njiani, na jinsi alivyotambulikana nao kwa kumega mkate.


Hawa wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja katika kuomba, pamoja nao wanawake, na Mariamu mama wake Yesu, na ndugu zake.


Nae, alipokwisha kufika na kuiona neema ya Mungu akafurahi, akawasihi wote waambatane na Bwana kwa kusudi la moyo.


wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya shidda nyingi.


Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kupokea chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe,


Akapanda juu tena, akamega mkate, akala, akazidi kuongea nao hatta alfajiri, ndipo akaenda zake.


Hatta siku ya kwanza ya juma, wanafunzi walipokusanyika illi kumega mkate, Paolo akawakhutubu, akaazimu kusafiri siku ya pili yake, akafuliza maneno yake mpaka nsiku wa manane.


Hatta walipofunguliwa, wakaenda kwa watu wao, wakawapasha khabari ya mambo yote waliyoambiwa na makuhani wakuu na wazee.


Hatta walipokwisha kumwomba Mungu, pahali paie walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa uthabiti.


na sisi tutadumu katika kumwomba Mungu na kulikhudumia Neno lake.


kwa tumaini, mkifurahi; katika shidda, mkivumilia; katika kusali, mkidumu;


Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani. Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani.


Tena nawasifu, ndugu, kwa sababu mmenikumbuka katika mambo yote, nanyi mmeyashika yale niliyowatolea vile vile kama nilivyowatolea.


Bassi, ndugu, nikija kwenu na kunena kwa lugha, nitawafaidia nini, isipokuwa nanena nanyi kwa njia ya ufunuo, au kwa njia ya elimu, au kwa njia ya khotuba, au kwa njia ya fundisho?


Nastaajabu kwa kuwa mmemwacha hivi upesi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo,


mmejengwa juu ya misingi ya mitume na manabii, na Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni;


kwa sala zote na kuomha mkisali killa wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo, mkifanya juhudi sana, na kuwaombea watakatifu wote,


kwa sababu ya ushirika wenu katika kuieneza Injili, tangu siku ya kwanza hatta leo hivi;


mkidumu tu katika imani, mmewekwa juu ya misingi, mkawa imara; msipogeuzwa na kuliacha tumaini la Injili mliyosikia khabari zake, iliyokhubiriwa katika viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu; ambayo mimi Paolo nalikuwa mkhudumu wake.


Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani,


Bali wewe ukae katika yale uliyofundishwa na kuhakikishwa, kwa maana unajua ni nani ambae ulijifunza kwake,


tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tukionyana; na tukizidi, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.


Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali miongoni mwao walio na imani ya kutuokoa roho zetu.


tuliyoiona na kuisikia, twawakhubiri ninyi; ninyi nanyi mpate kushirikiana na sisi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo.


bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu Kristo, Mwana wake, yatusafisha dhambi zote.


Walitoka kwetu, bali hawukuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka illi wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu.


Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imaui yenu iliyo takatifu, na kuomba katika Roho Mtakatifu,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo