Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 2:4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha mbalimbali, kama Roho alivyowajalia kutamka.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema lugha mbalimbali kadiri Roho alivyowawezesha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema lugha mbalimbali kadiri Roho alivyowawezesha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema lugha mbalimbali kadiri Roho alivyowawezesha.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Wote wakajazwa na Roho Mtakatifu wa Mungu, wakaanza kunena kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Wote wakajazwa na Roho wa Mwenyezi Mungu, wakaanza kunena kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia.

Tazama sura Nakili




Matendo 2:4
55 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini hapo wakatapowapelekeni, msifikirifikiri jinsi mtakavyosema; maana mtapewa saa ile mtakayosema.


Na ishara hizi zitafuatana nao waaminio; Kwa jina langu watafukuza pepo; watasema kwa ndimi mpya;


Kwa maani atakuwa mkuu mbele ya Mungu, hatakunywa divai wala kileo: nae atajazwa Roho Mtakatifu hatta tangu tumbo la mama yake.


Ikawa Elizabeti alipoisikia salamu ya Mariamu, mtoto mchanga akaruka ndani ya tumbo lake; Elizabeti akajazwa Roho Mtakatifu, akapaaza sauti yake kwa nguvu, akasema,


Zakaria babae akajazwa Roho Mtakatifu, akatabiri, akinena,


kwa kuwa Roho Mtakatifu atawafundisha saa hiyo hiyo yawapasavyo kuyanena.


Kwa maana mimi nitawapeni kinywa na hekima, ambayo watesi wenu hawataweza kuikana wala kushindana nayo.


NA Yesu, akijaa Roho Mtakatifu, akarudi kutoka Yordani: akaongozwa na Roho kwenda jangwani, akijaribiwa na Shetani muda wa siku arubaini.


Lakini Mfariji, Roho Mtakatifu, ambae Baba atampeleka kwa jina langu, yeye atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.


Akiisha kusema haya, akawapulizia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu.


ya kwamba Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi si nyingi.


Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemi, na katika Yahudi yote, na Samaria, na hatta mwisho wa inchi.


Kwa maana waliwasikia wakisema kwa lugha, wakimwadhimisha Mungu.


Ndipo Petro akajibu, Aweza mtu kuwakataza hawa maji, wasibatizwe, watu waliopokea Roho Mtakatifu vile vile kama sisi?


Ikawa nilipoanza kunena, Roho Mtakatifu akawashukia kama alivyotushukia sisi mwanzo.


Maana alikuwa mtu mwema, amejaa Roho Mtakatifu na imani: watu wengi wakajitia upande wa Bwana.


Na wanafunzi walijaa furaha na Roho Mtakatifu.


Lakini Saul ambae ndiye Paolo, akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho, akanena,


Na Mungu, ajuae mioyo ya watu, akawashuhudia, akiwapa Roho Mtakatifu vilevile kama alivyotupa sisi;


Na Paolo, alipokwisba kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri.


Wakrete na Waarabu; tunawasikia hawa wakisema kwa maneno yetu matendo makuu ya Mungu.


Kukawatokea ndimi zilizogawanyika, kama ndimi za moto uliowakalia killa mmoja wao.


Hatta walipokwisha kumwomba Mungu, pahali paie walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa uthabiti.


Ndipo Petro, akijaa Roho Mtakatifu, akawaambia,


Bassi ndugu, chagueni watu saba miongoni mwenu, walioshuhudiwa kuwa wema, illi tuwaweke juu ya jambo hili:


Neno hili likapendeza machoni jia mkutano wote: wakamehagua Stefano, mtu aliyejaa imani na Roho Mtakatifu na Filipo, na Prokoro, na Nikanor, na Timoni, na Parmena, na Nikolao mwongofu wa Antiokia.


Na Stefano, akijaa imani na uwezo, alikuwa akifanya maajabu na ishara kubwa katika watu.


Nae akijaa Roho Mtakatifu, akakaza macho yake, akitazama mbinguni, akauona utukufu wa Mungu, na Yesu akisimama mkono wa kuume wa Mungu.


Wakaweka mikono yao juu yao, nao wakapokea Roho Mtakatifu.


Anania akaenda zake, akaingia mle nyumbani; akamwekea mikono akisema, Ndugu Saul, Bwana amenipeleka, Yesu, yeye aliyekutokea katika njia uliyoijia, upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu.


Bassi Mungu wa tumaini awajazeni furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mataktifu.


na mwingine kutenda kazi za miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha;


NIJAPOSEMA kwa lugha za wana Adamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upato uvumao.


Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.


Namshukuru Mungu wangu, nanena kwa lugha zaidi ya ninyi nyote;


Nami nataka ninyi nyote mnene kwa lugha, lakini zaidi sana mpate kukhutubu; maana yeye akhutubuye ni mkuu kuliko yeye anenae kwa lugha, isipokuwa afasiri, illi kusudi Kanisa lipate kujengwa.


na kimjua upendo wake Kristo, ambao hauwezi kufahamiwa vema kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu.


Tena msilevye kwa mvinyo, kwa kuwa haina kiasi, bali mjazwe Roho;


kwa sala zote na kuomha mkisali killa wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo, mkifanya juhudi sana, na kuwaombea watakatifu wote,


Waliofunuliwa ya kuwa si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yetu walitumika katika mambo hayo, ambayo sasa yamekhubiriwa kwenu na wale waliowakhubiri ninyi Injili kwa Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni. Mambo hiayo malaika wanatamani kuyachuugulia.


Maana unabii haukuletwa zamani kwa mapenzi ya mwana Adamu; hali wana Adamu, watakatifu wa Mungu, walinena, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo