Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 2:38 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe killa mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

38 Petro akajibu, “Tubuni na kila mmoja wenu abatizwe kwa jina la Yesu Kristo ili mpate kuondolewa dhambi zenu na kupokea ile ahadi ya Roho Mtakatifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

38 Petro akajibu, “Tubuni na kila mmoja wenu abatizwe kwa jina la Yesu Kristo ili mpate kuondolewa dhambi zenu na kupokea ile ahadi ya Roho Mtakatifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

38 Petro akajibu, “Tubuni na kila mmoja wenu abatizwe kwa jina la Yesu Kristo ili mpate kuondolewa dhambi zenu na kupokea ile ahadi ya Roho Mtakatifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

38 Petro akawajibu, “Tubuni, mkabatizwe kila mmoja wenu kwa jina la Isa Al-Masihi, ili mpate kusamehewa dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

38 Petro akawajibu, “Tubuni, mkabatizwe kila mmoja wenu kwa jina la Isa Al-Masihi, ili mpate kusamehewa dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho wa Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili




Matendo 2:38
43 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi, enendeni, kawafanyeni mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;


Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.


wakabatizwa nae mtoni Yordani, wakiziungama dhambi zao.


Tokea wakati huo Yesu akaanza kukhubiri, na kusema, Tubuni, maana ufalme wa mbinguni umekaribia.


akineua, Wakati umetimia, na ufalme wa Muugu umekaribia; tubuni, kaiaminim injili.


Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.


na mataifa yote wakhubiriwe kwa jina lake toba na ondoleo la dhambi, kuanzia Yerusalemi.


Nao makutano wakamwuliza wakinena, Tufanyeni, bassi?


Huyu manabii wote humshuhudia, ya kwamba kwa jina lake killa amwaminiye atapewa ondoleo la dhambi.


Akaamuru wabatizwe kwa Jina lake Yesu Kristo. Ndipo wakamsihi azidi kukaa siku kadha wa kadha.


Bassi, ibainike kwenu, ndugu, ya kuwa kwa huyu mnakhubiriwa ondoleo la dhambi;


Hatta alipokwisha kumbatiza, yeye na nyumba yake, akatusihi, akisema, Kama mmeniona kuwa mwaminifu kwa Bwana, ingieni nyumbani mwangu mkakae; akatushurutisha.


Bassi zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hauoni; bali sasa anawakhuhiri watu wote wa killa mahali watubu.


nikiwashuhudia Wayahudi na Wayunani toba iliyo kwa Mungu, na imani iliyo kwa Bwana wetu Yesu Kristo.


Bassi sasa, unakawiliani? Simama ubatizwe ukaoshe dhambi zako, ukiliitia jina la Bwana.


uwafumhue macho yao, waiache giza na kuielekea nuru, na waziache nguvu za Shetani na kumwelekea Mungu, na wapate masamaha ya dhambi zao, na urithi miongoni mwao waliotakaswa kwa imani iliyo kwangu.


hali kwanza niliwakhubiri wale wa Dameski na Yerusalemi, na katika inchi yote ya Yahudi, na watu wa mataifa, watubu wakamwelekee Mungu, wakiyatenda matendo yanayopatana na kutubu kwao.


Tubuni bassi, mrejee, illi dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuhurudishwa kwa kuwako kwake Bwana:


Mtu kuyo Mungu amemtukuza kwa mkono wake wa kuume, awe Mkuu na Mwokozi, awape Waisraeli toha na masamaha ya dhambi.


Lakini walimpomwamini Filipo, akizikhubiri khabari njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake.


Petro akamwambia, Fedha yako na ipotelee mbali pamoja nawe, kwa kuwa umedhani ya kuwa karama ya Mungu yapatikana kwa mali.


Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Yesu Kristo, twalibatizwa katika mauti yake?


Katika yeye tuna ukombozi kwa damu yake, masamaha ya dhambi, kwa wingi wa neema yake;


alituokoa, si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda, bali kwa rehema yake, kwa josho la kuzaliwa kwa pili, na kufanywa upya na Roho Mtakatifu,


Mfano wa mambo haya ni ubatizo, nnaowaokoa na ninyi siku hizi; (sio kuwekea, mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu), kwa kufufuka kwake Yesu Kristo;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo