Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 2:30 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

30 Bassi kwa kuwa nabii, akijua ya kuwa Mungu amemwapia kwa kiapo, ya kwamba katika uzao wa viuno vyake kwa jinsi ya kiwiliwili atamwinua Kristo, akae katika kiti chake cha enzi; yeye mwenyewe

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

30 Lakini kwa vile Daudi alikuwa nabii, alijua kuwa Mungu alimwapia kiapo kwamba atamtawaza mmoja wa uzawa wake kuwa mfalme mahali pake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

30 Lakini kwa vile Daudi alikuwa nabii, alijua kuwa Mungu alimwapia kiapo kwamba atamtawaza mmoja wa uzawa wake kuwa mfalme mahali pake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

30 Lakini kwa vile Daudi alikuwa nabii, alijua kuwa Mungu alimwapia kiapo kwamba atamtawaza mmoja wa uzawa wake kuwa mfalme mahali pake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

30 Lakini alikuwa nabii na alijua ya kuwa Mungu alikuwa amemwahidi kwa kiapo, kwamba angemweka mmoja wa wazao wake penye kiti chake cha utawala.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

30 Lakini alikuwa nabii na alijua ya kuwa Mungu alikuwa amemwahidi kwa kiapo kwamba angemweka mmoja wa wazao wake penye kiti chake cha enzi.

Tazama sura Nakili




Matendo 2:30
37 Marejeleo ya Msalaba  

Akawaambia, Imekuwaje bassi Daud katika Roho kumwita Bwana, akinena,


Walipokwisha kumsulibi, wakagawa nguo zake, wakipiga kura: illi litimie neno lililonenwa na nabii. Waligawa nguo zangu kati yao, na juu ya vazi langu walipiga kura.


Kwa sababu Daud mwenyewe alisema, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, Bwana alimwambia Bwana wangu, Keti mkono wangu wa kuume Hatta niwafanyapo adui zako kuwa chini ya miguu yako.


Akawaambia, Haya ndiyo maneno yangu niliyowaambieni, nilipokuwa kwenu, ya kuwa hayana buddi kutimizwa yote niliyoandikiwa katika torati ya Musa, na katika manabii, na katika zaburi.


Ndugu imepasa andiko litimizwe, alilolinena Roho Mtakatifu zamani kwa kinywa cha Daud, katika khabari za Yuda, aliyekuwa kiongozi wao waliomkamata Yesu: kwa sababu alikuwa amehesabiwa pamoja na sisi,


khabari za Mwana wake, aliyekuwa katika ukoo wa Daud kwa jinsi ya mwili,


Na tena Isaya anena, Litakuwa shina la Yesse, Nae aondokeae kuwatawala Mataifa; ndiye Mataifa watakaemtumaini.


Mkumbuke Yesu Kristo, aliyefufuka katika wafu, wa uzao wa Daud, kama inenavyo injili yangu.


KWA sehemu nyingi na kwa namna nyingi Mungu zamani alisema na babu zetu katika manabii,


Kwa hiyo, kama anenavyo Robo Mtakatifu, Leo, kama mtasikia sauti yake,


aweka tena siku fullani, akisema katika Daud baada ya muda mwingi namna hii, Leo; kama ilivyonenwa tangu zamani, Leo kama mtasikia sauti yake, msiifanye migumu mioyo yenu.


Katika neno hilo Mungu, akitaka kuwaonyesha wairithio ile ahadi jinsi mashauri yake yasivyoweza kubadilika, alitia kiapo katikati;


(maana wale walifanywa makuhani pasipo kiapo; hali yeye, pamoja na kiapo, kwa yeye aliyemwambia, Bwana ameapa wala hataghairi, Wewe kuhani hatta milele kwa daraja la Melkizedeki;)


Maana unabii haukuletwa zamani kwa mapenzi ya mwana Adamu; hali wana Adamu, watakatifu wa Mungu, walinena, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.


Hawa watafanya vita na Mwana kondoo, na Mwana kondoo atawashinda, kwa maana ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme; nao walioitwa wateule, waaminifu, watashinda pamoja nae.


Nae ana jina limeandikwa katika vazi lake mi paja vake, MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo