Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 2:27 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

27 Kwa maana hutaniacha roho yangu katika kuzimu: Wala hutamtoa Mtakatifu wako aone uharibifu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 maana hutaiacha roho yangu kuzimu, wala kumruhusu mtakatifu wako aoze.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

27 maana hutaiacha roho yangu kuzimu, wala kumruhusu mtakatifu wako aoze.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 maana hutaiacha roho yangu kuzimu, wala kumruhusu mtakatifu wako aoze.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 Kwa maana hutaniacha kaburini, wala hutamwacha Aliye Mtakatifu wako kuona uharibifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

27 Kwa maana hutaniacha kaburini, wala hutamwacha Aliye Mtakatifu wako kuona uharibifu.

Tazama sura Nakili




Matendo 2:27
26 Marejeleo ya Msalaba  

Nawe Kapernaum, uliyeinuliwa hatta mbinguni, utashushwa hatta kuzimu: kwa maana kama miujiza iliyofanyika kwako, ingalifanyika katika Sodom, ungalikuwapo hatta leo.


akinena, Tʼuna nini nawe, Yesu Mnazareti? umekuja kutuangamiza? Nakutambua wewe, Mtakatifu wa Mungu.


Malaika akajibu, akamwambia, Roho Mtakatifu atakujia, na nguvu zake Aliye juu zitakutilia kivuli: kwa biyo kitakachozaliwa kitakwitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.


Bassi katika akhera akainua macho yake, akiwa katika adhabu, akamwona Ibrahimu yuko mbali, na Lazaro kifuani pake.


Akawaambia, Haya ndiyo maneno yangu niliyowaambieni, nilipokuwa kwenu, ya kuwa hayana buddi kutimizwa yote niliyoandikiwa katika torati ya Musa, na katika manabii, na katika zaburi.


Ah, tuna nini nawe Yesu Mnazareti? umekuja kutuangamiza? Nakutambua wewe, Mtakatifu wa Mungu.


Yesu akasema, Liondoeni jiwe. Martha, dada yake yule mtu aliyefariki, akamwambia, Bwana, ananuka sasa: maana amekuwa mayiti siku nne.


Kwa hiyo moyo wangu ukapendezwa, ulimi wangu ukafurahi; Tena mwili wangu nao utakaa katika matumaini.


Umenifundisha njia ya uzima; Utanijaza furaha kwa uso wako.


akitangulia kuyaona haya, alitaja khabari za kufufuka kwake Kristo, ya kama roho yake haikuachwa katika kuzimu, wala mwili wake hankuona uharibifu,


Ninyi mlimkana yule Mtakatifu, yule Mwenye haki, mkataka mpewe muuaji:


Maana ni kweli, Herode na Pontio Pilato pamoja na mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika juu ya mtumishi wako mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta,


kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa panda la mwisho; maana panda litalia, na wafu watafufuka, wasiwe na uharibifu, na sisi tutahadilika.


U wapi, mauti, uchungu wako? Ku wapi, kaburi, kushinda kwako?


Na ninyi mmepakwa mafuta nae aliye Mtakatifu na mnajua yote.


na aliye hayi; nami nalikuwa nimekufa, na tazama ni hayi hatta milele na milele. Amin. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.


Bahari ikawatoa wafu waliomo ndani yake. Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu walio ndani yake. Wakahukumiwa killa mtu kwa kadiri ya matendo yao.


Na kwa malaika wa kanisa lililo katika Filadelfia andika; Haya ayanena yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daud, mwenye kufungua wala hapana afungae, nae afunga wala hapana afuuguae.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo