Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 2:23 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

23 mtu huyu alitwaliwa nanyi kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa kujua kwake taugu zamani, nanyi mkamsulibisha kwa mikono mibaya, mkamwua:

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Kufuatana na mpango wake mwenyewe Mungu alikwisha amua kwamba Yesu angetiwa mikononi mwenu; nanyi mkamuua kwa kuwaachia watu wabaya wamsulubishe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Kufuatana na mpango wake mwenyewe Mungu alikwisha amua kwamba Yesu angetiwa mikononi mwenu; nanyi mkamuua kwa kuwaachia watu wabaya wamsulubishe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Kufuatana na mpango wake mwenyewe Mungu alikwisha amua kwamba Yesu angetiwa mikononi mwenu; nanyi mkamuua kwa kuwaachia watu wabaya wamsulubishe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Baada ya huyu mtu kutolewa kwenu kwa mpango wa Mungu uliokusudiwa kwa kujua kwake Mungu tangu zamani, ninyi mlimuua kwa kumsulubisha msalabani, kwa mikono ya watu waovu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Huyu mtu akiisha kutolewa kwa shauri la Mungu lililokusudiwa kwa kujua kwake Mwenyezi Mungu tangu zamani, ninyi, kwa mikono ya watu wabaya, mlimuua kwa kumgongomea msalabani.

Tazama sura Nakili




Matendo 2:23
39 Marejeleo ya Msalaba  

na watampeleka kwa Mataifa wapate kumdhihaki, na kumpiga mijeledi, na kumsulibi; na siku ya tatu atafufuka.


Mwana wa Adamu aenda zake, kama alivyoandikiwa: lakini ole wake mtu yule ambae Mwana wa Adamu anasalitiwa nae! Ingekuwa kheri kwake mtu yule kama asingalizaliwa.


Walipokwisha kumsulibi, wakagawa nguo zake, wakipiga kura: illi litimie neno lililonenwa na nabii. Waligawa nguo zangu kati yao, na juu ya vazi langu walipiga kura.


Wakamsulibi, wakagawanya nguo zake wakizipigia kura killa mtu atwae nini.


Kwa maana Mwana wa Adamu aenda zake kama ilivyoamriwa; lakini ole wake mtu yule ambae anasalitiwa nae!


Kwa maana nawaambieni, Hili lililoandikwa halina buddi kutimizwa kwangu, Alihesabiwa pamoja na maasi; kwa maana linipasalo lina mwisho.


Hatta walipofika pahali paitwapo Kichwa, ndiko walikomsulibisha, na wale wakhalifu, mmoja mkono wa kuume, na mmoja mkono wa kushoto.


na jinsi makuhani wakuu na wakubwa wetu walivyomtoa kwa hukumu ya kufa, wakamsulibisha;


wakamsulibisha huko, na wengine wawili pamoja nae, huko na huko, na Yesu katikati.


Bassi wakaambiana, Tusiipasue, lakini tuipigie kura, iwe ya nani; andiko litimie linenalo, Waligawanya nguo zangu, na vazi langu walilipigia kura. Bassi ndivyo walivyofanya askari.


Kwa maana wakaao Yerusalemi, na wakuu wao, kwa kuwa hawakumjua huyu, wala sauti za manabii wanaosomwa killa sabato, wamezitimiza kwa kumhukumu.


Kazi zake zote zimejulika na Mungu tangu mwanzo wa ulimwengu.


Bassi nyumba yote ya Israeli na wajue yakini ya kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo mliyemsulibisha kuwa Bwana na Kristo.


Lakini mambo yale aliyokhubiri Mungu tangu zamani kwa vinywa vya manabii wake wote, ya kama Kristo atateswa, ameyatimiza hivyo.


illi wafanye yote ambayo mkono wako na mashauri yako yamekusudia tangu zamani yatokee.


Je! hatukuwaamuru ninyi kwa nguvu, msifundishe kwa jina hili: nanyi mmeijaza Yerusalemi mafundisho yenu, na mnataka kuleta damu ya mtu yule juu yetu.


Mungu wa baba zetu alimfufua Yesu, ambae ninyi mlimwua mkamtundika katika mti.


Ni yupi katika manabii ambae baba zenu hawakumwudhi? nao waliwaua wale waliotabiri khabari za kuja kwake yule mwenye haki; ambae ninyi sasa mmemsaliti mkamwua;


Kwa kuwa wote waliokosa pasipo sharia watapotea pasipo sharia, na wote waliokosa, wakiwa na sharia, watahukumiwa kwa sharia.


(kama ilivyoandikwa, Nimekuweka kuwa baba wa mataifa mengi) mbele zake aliyemwamini, yaani Mungu, mwenye kuwahuisha wafu, avitajae vitu visivyokuwa kana kwamba vimekuwa.


waliomwua Bwana Yesu na manabii wao wenyewe na kutuudhi sisi, wala hawampendezi Mungu, wala hawapatani na watu wo wote;


kama vile Mungu alivyotangulia kuwajua tangu milele katika utakaso wa Roho, hatta wakapata kutii na kunyunyizwa damu ya Yesu Kristo; Neema na amani ziongezwe kwenu.


aliyejuliwa tangu zamani, kabla haijawekwa misingi ya dunia; lakini alifimuliwa mwisho wa zamani kwa ajili yenu,


tena, Jiwe lakujikwaza mguu, na mwamba wa kujiangusha; maana hujikwaza kwa neno lile, wakiliasi, nao waliwekwa wapate hayo.


Kwa maana kuna watu wamejiingiza kwa siri, watu walioandikiwa zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufasiki, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo.


Watu wote wakaao juu ya inchi wakamsujudu, ambao majina yao hayakuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana kondoo aliyechinjwa kabla ya kuwekwa misingi ya dunia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo