Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 2:22 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

22 Enyi waume wa Israeli, sikieni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 “Wananchi wa Israeli, sikilizeni maneno haya! Yesu wa Nazareti alikuwa mtu ambaye mamlaka yake ya kimungu yalithibitishwa kwenu kwa miujiza, maajabu na ishara Mungu alizofanya kati yenu kwa njia yake, kama mnavyojua.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 “Wananchi wa Israeli, sikilizeni maneno haya! Yesu wa Nazareti alikuwa mtu ambaye mamlaka yake ya kimungu yalithibitishwa kwenu kwa miujiza, maajabu na ishara Mungu alizofanya kati yenu kwa njia yake, kama mnavyojua.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 “Wananchi wa Israeli, sikilizeni maneno haya! Yesu wa Nazareti alikuwa mtu ambaye mamlaka yake ya kimungu yalithibitishwa kwenu kwa miujiza, maajabu na ishara Mungu alizofanya kati yenu kwa njia yake, kama mnavyojua.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 “Enyi Waisraeli, sikilizeni maneno haya nisemayo: Isa Al-Nasiri alikuwa mtu aliyethibitishwa kwenu na Mungu kwa miujiza, maajabu na ishara, ambayo Mungu alitenda miongoni mwenu kupitia kwake, kama ninyi wenyewe mjuavyo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 “Enyi Waisraeli, sikilizeni maneno haya nisemayo: Isa Al-Nasiri alikuwa mtu aliyethibitishwa kwenu na Mwenyezi Mungu kwa miujiza, maajabu na ishara, ambayo Mungu alitenda miongoni mwenu kupitia kwake, kama ninyi wenyewe mjuavyo.

Tazama sura Nakili




Matendo 2:22
42 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini mimi nikifukuza pepo kwa uweza wa Bobo ya Mungu, bassi ufalme wa Mungu umekujieni.


akaenda, akakaa mji uliokwitwa Nazareti: illi litimie neno lililonenwa na manabii, Atakwitwa Mnazorayo.


Makutano wakimwona, wakastaajabu, wakamtukuza Mungu, aliyewapa watu mamlaka ya jinsi hii.


Lakini nikifukuza pepo kwa kidole cha Mungu, bassi ufalme wa Mungu umewajieni.


Wakamweleza, Yesu wa Nazareti anapita.


Akajibu mmoja wao, jina lake Kleopa, akamwambia, Je! wewe peke yako u mgeni katika Yerusalemi, usiyajue yaliyokuwa ndani yake siku hizi?


Filipo akamwona Nathanaeli, akamwambia, Tumemwona yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati, na na manabii, Yesu, mwana wa Yusuf, mtu wa Nazareti


Kama sizitendi kazi za Baba yangu, msiniamini;


Bassi makuhani wakuu na Mafarisayo wakakusanya baraza, wakanena, Tunafanya nini? Maana mtu huyu afanya ishara nyingi.


Bassi wakamshuhudia makutano waliokuwa pamoja nae alipomwita Lazaro kutoka kaburini akamfufua.


Kama singalitenda kazi kwao asizozitenda mtu mwingine, wasingalikuwa na dhambi; sasa wametuona mimi na Baba yangu, na kutuchukia.


Pilato akaandika anwani, akaiweka juu ya msalaba, imeandikwa, YESU MNAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI.


huyu alikuja kwa Yesu usiku, akamwambia, Rabbi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezae kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, illa Mungu awe pamoja nae.


Bassi Yesu akamwambia, Msipoona ishara na maajabu hamtaamini kabisa.


Lakini ushuhuda nilio nao ni mkubwa kuliko ule wa Yohana: kwa kuwa zile kazi nilizopewa na Baba nizimalize, kazi hizo zenyeye ninazozitenda zinanishuhudia kwamba Baba amenituma.


Bassi watu wale, walipoiona ishara aliyoifanya Yesu, wakasema, Huyu hakika ni nabii yule ajae ulimwenguni.


Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hatta uzima wa milele, Mwana wa Adamu atakachowapeni: maana huyu ndiye aliyetiwa muhuri na Baba, yaani, Mungu.


Watu wengi katika makutano wakamwamini: wakasema, Atakapokuja Kristo, je! atafanya ishara nyingi zaidi kuliko hizi alizozifanya huyu?


Kama huyu asingalitoka kwa Mungu, asingeweza kutenda neno.


Paolo akasimama, akawtipungia mkono, akanena, Enyi wanme wa Israeli, na ninyi mnaomcha Mungu, sikilizeni.


Hatta walipolika wakalikutanisha Kanisa, wakawaeleza mambo yote aliyoyafanya Mungu pamoja nao, na ya kwaruba amewafungulia mataifa mlango wa imani.


Nitatoa ajabu katika mbingu juu, Na ishara katika inchi chini, Damu na moto, na mvuke wa moshi:


Killa mtu akaingiwa na khofu: ajabu nyingi na ishara zikafanyika kwa ujumbe wa mitume.


Huyu ndiye mtu yule afundishae watu katika killa mahali kinyume cha taifa letu na torati na pahali hapa. Tena, zaidi ya haya, amewaingiza Wayunani katika hekalu, akapatia najis pahali hapa palakatifu.


Nikajibu Wewe nani Bwana? Akaniambia, Mimi ni Yesu Mnazareti, ambae wewe unaniudhi.


Kwa maana tamemwona mtu huyu mkorofi, muanzishaji wa fitina katika Mayahudi waliomo duniani, tena ni kichwa cha uzushi wa Wanazorayo.


Kwa maana mfalme anajua khabari za mambo haya, na naweza kusema nae bila khofu, kwa sababu najua sana ya kuwa hapana neno moja katika hayo asilolijua; kwa maana jambo hilo halikutendeka pembeni.


Kweli, mimi mwenyewe naliona ndani ya nafsi yangu kwamba yanipasa kutenda mambo mengi yaliyopingamana na jina lake Yesu Mnazareti;


Hatta Petro alipoona haya akawajibu watu, Enyi Waisraeli, mbona mnastaajabia haya, au mbona mnatukazia macho sisi, kana kwamba tumemfanya huyu aende kwa nguvu zetu sisi, au kwa utawa wetu sisi?


Petro akanena, Fedha sina, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Mnazareti, simama uende.


jueni ninyi nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa kwa jina la Yesu Mnazareti, ambae ninyi mlimsulibisha, Mungu akamfufua, kwa jina hilo mtu huyu anasimama mzima mbele yenu.


akaamuru mitume wawekwe nje kitambo, akawaambia, Enyi waume wa Israeli, jihadharini jinsi mtakavyowatenda watu hawa.


maana tumemsikia akisema kwamba Yesu huyo Mnazareti atapaharibu pahali hapa, na kuzihadili desturi tulizopewa na Musa.


Maana ishara za mtume zilitendwa kati yenu katika uvumilivu wote, kwa ishara na maajabu na nguvu.


Mungu nae akishuhudu pamoja nao kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi, na kwa karama za Roho Mtakatifu, kama alivyopenda mwenyewe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo