Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 2:17 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

17 Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, Nitawamwagia watu wote Roho yangu, Na wana wenu na binti zenu watatabiri, Na vijana wenu wataona maono: Na wazee wenu wataota ndoto:

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 ‘Katika siku zile za mwisho, asema Bwana, nitawamiminia binadamu wote Roho wangu. Watoto wenu wa kiume na wa kike watatoa unabii, vijana wenu wataona maono, na wazee wenu wataota ndoto.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 ‘Katika siku zile za mwisho, asema Bwana, nitawamiminia binadamu wote Roho wangu. Watoto wenu wa kiume na wa kike watatoa unabii, vijana wenu wataona maono, na wazee wenu wataota ndoto.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 ‘Katika siku zile za mwisho, asema Bwana, nitawamiminia binadamu wote Roho wangu. Watoto wenu wa kiume na wa kike watatoa unabii, vijana wenu wataona maono, na wazee wenu wataota ndoto.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 “ ‘Katika siku za mwisho, asema Mungu, nitamimina Roho wangu juu ya wote wenye mwili. Wana wenu wa kiume na wa kike watatabiri, vijana wenu wataona maono, na wazee wenu wataota ndoto.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 “ ‘Katika siku za mwisho, asema Mungu, nitamimina Roho wangu juu ya wote wenye mwili. Wana wenu na binti zenu watatabiri, vijana wenu wataona maono, na wazee wenu wataota ndoto.

Tazama sura Nakili




Matendo 2:17
38 Marejeleo ya Msalaba  

Na wote wenye mwili watanona wokofu wa Mungu.


kama vile ulivyompa mamlaka juu ya killa mwenye mwili, illi yote uliyompa awape uzima wa milele.


Neno hili alilisema katika khabari ya Roho, ambae wale wamwaminio watampokea khalafu: kwa maana Roho Mtakatifu alikuwa bado kuwapo, kwa sababu Yesu alikuwa bado kutukuzwa.


Na wale waliotahiriwa walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu mataifa nao wameshukiwa kipaji cha Roho Mtakatifu.


Siku zizo hizo manabii walitelemka kutoka Yemsalemi hatta Antiokia.


Akasimama mmojawapo wao, jina lake Agabo, akaonyesha kwa nweza wa Roho Mtakatifu kwamba njaa kubwa itakuja karibu katika dunia nzima; nayo ikatukia katika siku za Klaudio Kaisari.


lakini jambo hili ni lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yoel:


Na siku zile nitawamwagia watumishi wangu wanaume na wauawake Roho yangu, Nao watatabiri,


Bassi akiisha kupandishwa hatta mkono wa kuume wa Mungu, na kupokea kwa Baba ile ahadi ya Roho Mtakatifu amekimwaga kitu hiki mnachokiona sasa na kukisikia.


Mtu huyu alikuwa na binti wane, mabikira, waliotabiri.


na tumaini halitahayarishi, kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepcwa sisi.


na mwingine kutenda kazi za miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha;


Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kiisha miujiza, kiisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na kutawala, na aina za lugha.


mwisho wa siku bizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi yote, kwa yeye aliufanya ulimwengu.


Dhahabu yenu na fedha yenu zimeingia kutu, na kutu yake itakushuhudieni, nayo itakula miili yenu kama moto. Mmejiwekea akiba katika siku hizi za mwisho.


Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho watakuja watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo