Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 2:11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

11 Wakrete na Waarabu; tunawasikia hawa wakisema kwa maneno yetu matendo makuu ya Mungu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Wayahudi na watu walioongokea dini ya Kiyahudi; wengine wametoka Krete na Arabia. Sisi sote tunasikia wakisema kwa lugha zetu wenyewe mambo makuu ya Mungu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Wayahudi na watu walioongokea dini ya Kiyahudi; wengine wametoka Krete na Arabia. Sisi sote tunasikia wakisema kwa lugha zetu wenyewe mambo makuu ya Mungu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Wayahudi na watu walioongokea dini ya Kiyahudi; wengine wametoka Krete na Arabia. Sisi sote tunasikia wakisema kwa lugha zetu wenyewe mambo makuu ya Mungu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 (Wayahudi na wale walioongokea dini ya Kiyahudi), Wakrete na Waarabu: sote tunawasikia watu hawa wakisema mambo makuu ya ajabu ya Mungu katika lugha zetu wenyewe.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Wayahudi na waongofu, Wakrete na Waarabu, sote tunawasikia watu hawa wakisema mambo makuu ya ajabu ya Mungu katika lugha zetu wenyewe.”

Tazama sura Nakili




Matendo 2:11
36 Marejeleo ya Msalaba  

Frugia na Pamfulia, Misri na pande za Libua karibu na Kurene, na Warumi wageni, Wayahudi na Waongofu,


Wakashangaa wote wakaingiwa na mashaka, wakaambiana, Maana yake nini mambo haya?


Na kwa sababu bandari haikukaa vema, watu wakae ndani yake wakati wa haridi, walio wengi wakatoa shauri tutweke tukatoke huko illi wapate kufika Foiniki, kama ikiwezekana, na kukaa huko wakati wa baridi: nayo ni bandari ya Krete, inaelekea kaskazini-mashariki na kusini-mashariki.


Na upepo wa kusi ulipoanza kuvuma kidogo, wakidhani ya kuwa wamepata walioazimu kupata, wakangʼoa nanga, wakasafiri karibu na Krete pwani kwa pwani.


Tukasafiri pole pole kwa muda wa siku nyingi, tukafika hatta Knido kwa shidda; na kwa sababu upepo ulikuwa ukituzuia tukapita chini ya Krete illi kuukinga upepo, tukaikabili Salmone.


na mwingine kutenda kazi za miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha;


Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kiisha miujiza, kiisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na kutawala, na aina za lugha.


wala sikupanda kwenda Yerusalemi kwa hao waliokuwa mitume kabla yangu, bali nalikwenda zangu Arabuni nikarudi teua Dameski.


Maana Hajir ni mlima Sinai ulioko Arabuni, umelingana na Yerusalemi wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na watoto wake.


Mtu wa kwao, nabii wao wenyewe, amesema. Wakrete ni wawongo siku zote, nyama mwitu wahaya, walafi, wasiofanya kazi. Ushuhuda huu ni kweli.


Kwa sababu hii nalikuaeba katika Krete, illi nyatengeneze yaliyosalia, na kuweka wazee katika killa mji kama nilivyokuamuru;


Mungu nae akishuhudu pamoja nao kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi, na kwa karama za Roho Mtakatifu, kama alivyopenda mwenyewe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo