Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 19:9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

9 Lakini wengine walikaidi, wakakataa kuamini, wakiitukana ile Njia mbele ya mkutano; bassi, akaondoka akawaacha, akawatenga wanafunzi nao, akahujiana na watu killa siku katika darasa ya mtu mmoja, jina lake Tyranno.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Lakini wengine walikuwa wakaidi, wakakataa kuamini, wakaanza kuongea vibaya juu ya hiyo njia ya Bwana katika kusanyiko la watu. Hapo Paulo alivunja uhusiano nao, akawachukua pembeni wale wanafunzi wake, akawa anazungumza nao kila siku katika jumba la masomo la Turano.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Lakini wengine walikuwa wakaidi, wakakataa kuamini, wakaanza kuongea vibaya juu ya hiyo njia ya Bwana katika kusanyiko la watu. Hapo Paulo alivunja uhusiano nao, akawachukua pembeni wale wanafunzi wake, akawa anazungumza nao kila siku katika jumba la masomo la Turano.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Lakini wengine walikuwa wakaidi, wakakataa kuamini, wakaanza kuongea vibaya juu ya hiyo njia ya Bwana katika kusanyiko la watu. Hapo Paulo alivunja uhusiano nao, akawachukua pembeni wale wanafunzi wake, akawa anazungumza nao kila siku katika jumba la masomo la Turano.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Lakini baadhi yao wakakaidi; walikataa kuamini, na wakakashifu Njia Ile hadharani. Basi Paulo aliachana nao. Akaenda na wanafunzi wale, akahojiana nao kila siku katika darasa la Tirano.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Lakini baadhi yao walikaidi. Walikataa kuamini, na wakakashifu ujumbe wake mbele ya umati wa watu. Basi Paulo aliachana nao. Akawachukua wanafunzi naye, akahojiana nao kila siku katika darasa la Tirano.

Tazama sura Nakili




Matendo 19:9
39 Marejeleo ya Msalaba  

Waacheni hawo; ni vipofu, viongozi wa vipofu. Na kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, watatumhukia shimoni wote wawili.


Kizazi kibaya na cha zina chataka ishara; wala hakitapewa ishara, isipokuwa ishara ya nabii Yunus. Akawaacha, akaenda zake.


Saa ile Yesu akawaambia makutano, Je, mmetoka, mfano wa watu wafukuzao mnyangʼanyi mna panga na marungu, kunitwaa? Killa siku naliketi mbele zenu hekaluni, nikifundisha, wala hamkunikamata.


Amewapofusba macho, amefanya migumu mioyo yao, Wasije wakaona kwa macho yao, wakafahamu kwa mioyo yao, Wakagenka, nikawaponya.


Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hajio Antiokia.


Lakini jamii ya watu wa mjini wakagawanyikana: bawa walikuwa upande wa Wayahudi, na hawa upande wa Mitume.


Wengine wakaamini, wakasuhubiana na Paolo na Sila; na Wayunani waliomcha Mungu, wengi sana, na wanawake wenye eheo si wachache.


Hatta wakati huo kukatukia ghasia si haba katika khabari ya Njia ile.


Na Paolo alipotaka kuingia kati ya watu, wanafunzi hawakumwacha aingie.


Kwa biyo kesheni, mkikumbuka kama miaka mitatu, usiku na mchana, sikuacha kumwonya killa mtu kwa machozi.


nikawaudhi watu wa Njia hii kiasi cha kuwaua, nikawafunga, nikiwatia gerezani, wanaume na wanawake.


isipokuwa kwa ajili ya sauti hii moja, nilipolia nikisimama katikati yao, Kwa ajili ya ufufuo wa wafu ninahukumiwa mbele yenu hivi leo.


Lakini tunataka kusikia kwako uonavyo wewe; kwa maana katika khabari za madhehebu hiyo tumekwisha kujua kwamba inanenwa vibaya kilia mahali.


Enyi wenye shingo gumu, msiotahiriwa mioyo wala masikio, siku zote mnampinga Roho Mtakatifu; kama baba zenu walivyofanya na ninyi vivyo hivyo.


akataka ampe khati za kwenda Dameski zilizoandikwa kwa masunagogi, illi akiona watu wa Njia hii, waume kwa wake, awafunge na kuwaleta Yerusalemi.


Imekuwaje bassi? Kitu kile ambacho Israeli alikuwa akikitafuta hakukipata, lakini wale waliochaguliwa walikipata, na wengine walitiwa ugumu.


Bassi, kama ni hivyo, atakae (kumrehemu) humrehemu, na atakae kumfanya mgumu humfanya mgumu.


kwa maana nimefunguliwa mlango mkubwa wa kufaa sana, na wengi wako wanipingao.


na majadiliano ya watu walioharibiwa akili zao, walioikosa kweli, wakidhani ya kuwa utawa ni njia ya kupata faida; ujitenge na watu kama hao,


Wajua hili, ya kuwa wote walio katika Asia wameniacha, katika hao ni Figello na Hermogene.


wenye mfano wa utawa, lakini wakikana nguvu zake; ujiepushe na hao.


likhubiri neno, fanya bidii, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, kaonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.


Lakini muonyane killa siku, maadam iitwapo leo; mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi.


Lakini hawo kama nyama wasio na akili, kwa asili yao watu wa kukamatwa kama nyama na kupotezwa, wakikufuru katika mambo wasiyoyajua, wataangamizwa katika maangamizo yao;


Na wengi watafuata jeuri zao; kwa hawo njia ya kweli itanenwa unajisi.


Lakini watu hawa huyatukana mambo wasiyoyajua, na mambo wayatambuayo kwa asili wajiharibu kwayo kama nyama wasio na akili.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo