Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Matendo 19:35 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

35 Na karani wa mji alipokwisha kuwatuliza watu, akasema, Enyi wanaume wa Efeso, ni mtu gani asiyejua ya kuwa mji wa Efeso ni mtunzaji wa hekalu ya Artemi, mungu mke aliye mkuu, na wa kitu kile kilichoanguka kutoka mbinguni?

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

35 Hatimaye karani wa mji alifaulu kuwanyamazisha, akawaambia, “Wananchi wa Efeso, kila mtu anajua kwamba mji huu wa Efeso ni mlinzi wa nyumba ya mungu Artemi na mlinzi wa ile sanamu iliyoanguka kutoka mbinguni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

35 Hatimaye karani wa mji alifaulu kuwanyamazisha, akawaambia, “Wananchi wa Efeso, kila mtu anajua kwamba mji huu wa Efeso ni mlinzi wa nyumba ya mungu Artemi na mlinzi wa ile sanamu iliyoanguka kutoka mbinguni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

35 Hatimaye karani wa mji alifaulu kuwanyamazisha, akawaambia, “Wananchi wa Efeso, kila mtu anajua kwamba mji huu wa Efeso ni mlinzi wa nyumba ya mungu Artemi na mlinzi wa ile sanamu iliyoanguka kutoka mbinguni.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

35 Baadaye karani wa mji akanyamazisha umati ule wa watu na kusema, “Enyi watu wa Efeso, je, ulimwengu wote haujui ya kuwa mji wa Efeso ndio unaotunza hekalu la Artemi aliye mkuu na ile sanamu yake iliyoanguka kutoka mbinguni?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

35 Baadaye karani wa mji akaunyamazisha ule umati wa watu na kusema, “Enyi watu wa Efeso, je, ulimwengu wote haujui ya kuwa mji wa Efeso ndio unaotunza hekalu la Artemi aliye mkuu na ile sanamu yake iliyoanguka kutoka mbinguni?

Tazama sura Nakili

Matendo 19:35
9 Marejeleo ya Msalaba  

Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi: bali mtu akiwa mcha Mungu, na kufanya mapenzi yake, huyo amsikia.

Wakalika Efeso, akawaacha huko. Yeye mwenyewe akaingia katika sunagogi, akahujiana na Wayahudi.

Tena mnaona na kusikia ya kwamba si katika Efeso tu, bali katika Asia yote pia, Paolo huyo amewaaminisha watu wengi na kuwageuza nia zao, akisema ya kwamba miungu inayofanywa kwa mikono siyo Mungu.

Lakini walipotambua ya kuwa yeye ni Myahudi, wakapiga kelele wote pia kwa sauti moja kwa muda wa saa mbili au karibu, wakilia, Artemi wa Waefeso ni mkuu.

Bassi kwa kuwa mambo haya hayawezi kukanushwa, imewapaseni kutulia, msifanye neno la haraka haraka.

kwamba zamani zile mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni, wasio wa maagano ya ahadi; mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani.

kwa unafiki wa watu wasemao uwongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;

Tufuate:

Matangazo

Matangazo