Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Matendo 19:34 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

34 Lakini walipotambua ya kuwa yeye ni Myahudi, wakapiga kelele wote pia kwa sauti moja kwa muda wa saa mbili au karibu, wakilia, Artemi wa Waefeso ni mkuu.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

34 Lakini walipotambua kuwa yeye ni Myahudi, wote kwa sauti moja walipiga kelele: “Mkuu ni Artemi wa Efeso!” Wakaendelea kupayukapayuka hivyo kwa muda wa saa mbili.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

34 Lakini walipotambua kuwa yeye ni Myahudi, wote kwa sauti moja walipiga kelele: “Mkuu ni Artemi wa Efeso!” Wakaendelea kupayukapayuka hivyo kwa muda wa saa mbili.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

34 Lakini walipotambua kuwa yeye ni Myahudi, wote kwa sauti moja walipiga kelele: “Mkuu ni Artemi wa Efeso!” Wakaendelea kupayukapayuka hivyo kwa muda wa saa mbili.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

34 Lakini walipotambua kwamba alikuwa Myahudi, wote wakapiga kelele kwa sauti moja kwa karibu muda wa saa mbili, wakisema, “Artemi wa Efeso ni mkuu!”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

34 Lakini walipotambua kwamba alikuwa Myahudi, wote wakapiga kelele kwa sauti moja kwa karibu muda wa saa mbili, wakisema, “Artemi wa Efeso ni mkuu!”

Tazama sura Nakili

Matendo 19:34
10 Marejeleo ya Msalaba  

Mkiwa katika kusali, msipayukepayuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi.

wakawachukua kwa makadhi, wakasema, Watu hawa wanataharakisha mji wetu, nao ni Wayahudi.

Kwa maana mtu mmoja, jina lake Demetrio, mfua fedha, kazi yake kufanya vihekalu vya fedha vya Artemi, alikuwa akiwapatia mafundi faida nyingi.

Tena mnaona na kusikia ya kwamba si katika Efeso tu, bali katika Asia yote pia, Paolo huyo amewaaminisha watu wengi na kuwageuza nia zao, akisema ya kwamba miungu inayofanywa kwa mikono siyo Mungu.

Waliposikia haya wakajaa hasira, wakapiga kelele, wakisema, Artemi wa Waefeso m mkuu.

Wakatoa Iskander katika mkutano, Wayahudi wakimweka mbele ya watu. Iskander akawapungia mkono, akitaka kuwapa wale watu majibu.

Na karani wa mji alipokwisha kuwatuliza watu, akasema, Enyi wanaume wa Efeso, ni mtu gani asiyejua ya kuwa mji wa Efeso ni mtunzaji wa hekalu ya Artemi, mungu mke aliye mkuu, na wa kitu kile kilichoanguka kutoka mbinguni?

Wewe usemae kwamba mtu asizini, wazini mwenyewe? Wewe uchukiae sanamu, wateka mahekidu?

Wakamsujudu yule joka aliyempa nyama uwezo, wakamsujudu yule nyama, wakisema, Nani afananae na nyama? Nani awezae kufanya vita nae?

Tufuate:

Matangazo

Matangazo