Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 19:29 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

29 Mji wote ukajaa ghasia, wakaenda mbio wakaingia theatro kwa moyo mmoja, wakiisha kuwakamata Gaio na Aristarko, watu wa Makedonia waliosafiri pamoja na Paolo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

29 Mji wote ukajaa ghasia. Wakawavamia Gayo na Aristarko, wenyeji wa Makedonia, ambao walikuwa wasafiri wenzake Paulo, wakakimbia nao mpaka kwenye ukumbi wa michezo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

29 Mji wote ukajaa ghasia. Wakawavamia Gayo na Aristarko, wenyeji wa Makedonia, ambao walikuwa wasafiri wenzake Paulo, wakakimbia nao mpaka kwenye ukumbi wa michezo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

29 Mji wote ukajaa ghasia. Wakawavamia Gayo na Aristarko, wenyeji wa Makedonia, ambao walikuwa wasafiri wenzake Paulo, wakakimbia nao mpaka kwenye ukumbi wa michezo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

29 Mara mji wote ukajaa ghasia. Watu wakawakamata Gayo na Aristarko, wenyeji wa Makedonia waliokuwa wakisafiri na Paulo, wakakimbilia nao katika ukumbi wa maonesho.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

29 Mara mji wote ukajaa ghasia. Wakawakamata Gayo na Aristarko, watu wa Makedonia waliokuwa wakisafiri pamoja na Paulo, na watu wakakimbilia katika ukumbi wa michezo kama mtu mmoja.

Tazama sura Nakili




Matendo 19:29
19 Marejeleo ya Msalaba  

Na walipokuwa katika Salamini wakalikhubiri neno la Bwana katika masunagogi ya Wayahudi, nao walikuwa nae Yohana kuwakhudumia.


Siku ya pili tukafika Neapoli na kutoka hapo tukafika Filippi, mji wa Makedonia, mji ulio mkuu katika wilaya ile, nayo ni Kolonia ya Kirumi; tukawa katika mji huu, tukikaa siku kadha wa kadha.


Paolo akatokewa na maono usiku; alimwona mtu wa Makedonia amesimama, akimsihi akimwambia, Vuka uje Makedonia utusaidie.


Wakautabarakisha nle mkutano na wakubwa wa mji walipoyasikia hayo.


Mambo hayo yalipokwisha kumalizika, Paolo akaazimu rohoni mwake kupita kati ya Makedonia na Akaia aende Yerusalemi, akisema, Baada ya kuwako huko, yanipasa kuuona na Rumi.


Akatuma watu wawili miongoni mwa wale waliomkhudumia kwenda Makedonia, nao ni Timotheo na Erasto, yeye mwenyewe akakaa katika Asia kitambo.


Bassi wengine walikuwa wakilia hivi na wengine hivi: kwa maana ule mkutano umekwisha kuchafukachafuka, na walio wengi hawakuijua sababu ya kukusanyika kwao pamoja.


Ninyi wenyewe mnajua ya kuwa mikono hii imetumika kwa mahitaji yangu na yao walio pamoja nami.


Watu hawa wakafuataua nae mpaka Asia, Sopater Mberoya, na Aristarko na Sekundo, watu wa Thessalonika, na Gayo mtu wa Derbe, na Tukiko na Trofumo watu wa Asia.


Mji wote ukataharuki, watu wakakutanika mbio mbio, wakamkamata Paolo, wakamwokota, wakamtoa hekaluni; marra milango ikafungwa.


Wewe si vnle Mmisri ambae kabla ya siku hizi aliwafitinisha wale watu elfu nne, walioitwa Wauaji, akawaongoza jangwani?


Tukapanda katika merikebu ya Adramuttio iliyokuwa tayari kusafiri hatta miji ya pwani za Asia, tukatweka; Aristarko, Mmakedoni wa Thessalonika, akiwa pamoja nasi.


Gayo, mwenyeji wangu na wa Kanisa lote pia awasalimu. Erasto, wakili wa mji awasalimu, na Kwarto, ndugu yetu.


An mlibatizwa kwa jina la Paolo?


Maana nadhani ya ku wa Mungu ametutoa sisi mitume mwisho kama watu waliohukumiwa wauawe; kwa sababu tumekuwa tamasha kwa dunia na malaika na wana Adamu.


Wala si hivyo tu, bali alichaguliwa na makanisa asafiri pamoja nias katika jambo la neema hii inayokhudumiwa nasi, illi Bwana atukuzwe, ikadhihirike ya kuwa mioyo yenu ilikuwa tayari.


Aristarko, aliyefumgwa pamoja nami, awasalimu, na Marko, mjomba wake Barnaba, amhae mmepokea maagizo kwa khabari yake; akifika kwenu mkaribisheni.


na Marko, na Aristarko, na Dema, na Luka, watendao kazi pamoja nami.


MZEE kwa Gaio mpenzi, nimpendae katika kweli.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo