Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Matendo 19:27 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

27 Si kwamba kazi hii yetu ina khatari ya kudharauliwa, bassi; bali na hekalu ya mungu mke aliye mkuu kuhesabiwa si kitu, na kuondolewa utukufu wake, ambae Asia yote pia na walimwengu wote humwtihudu.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 Hivyo iko hatari kwamba biashara yetu itakuwa na jina baya. Si hivyo tu, bali pia jambo hilo linaweza kuifanya nyumba ya mungu Artemi kuwa si kitu cha maana. Hatimaye sifa zake huyo ambaye Asia na dunia yote inamwabudu, zitakwisha.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

27 Hivyo iko hatari kwamba biashara yetu itakuwa na jina baya. Si hivyo tu, bali pia jambo hilo linaweza kuifanya nyumba ya mungu Artemi kuwa si kitu cha maana. Hatimaye sifa zake huyo ambaye Asia na dunia yote inamwabudu, zitakwisha.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 Hivyo iko hatari kwamba biashara yetu itakuwa na jina baya. Si hivyo tu, bali pia jambo hilo linaweza kuifanya nyumba ya mungu Artemi kuwa si kitu cha maana. Hatimaye sifa zake huyo ambaye Asia na dunia yote inamwabudu, zitakwisha.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 Kwa hiyo kuna hatari si kwa kazi yetu kudharauliwa tu, bali pia hata hekalu la mungu wa kike Artemi aliye mkuu, anayeabudiwa jimbo lote la Asia na ulimwengu wote, litakuwa limepokonywa fahari yake ya kiungu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

27 Kwa hiyo kuna hatari si kwa kazi yetu kudharauliwa tu, bali pia hata hekalu la mungu mke Artemi, aliye mkuu, anayeabudiwa Asia yote na ulimwengu wote, litakuwa limepokonywa fahari yake ya kiungu.”

Tazama sura Nakili

Matendo 19:27
11 Marejeleo ya Msalaba  

Ole wenu waandisbi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mnakula nyumba za wajane, na kwa unafiki mnasali sala ndefu; kwa hiyo mtapokea hukumu iliyo kubwa mno.

Na injili hii ya ufalme itakhubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; ndipo ule mwisho utakapokuja.

Mambo haya yakaendelea kwa muda wa miaka miwili, hatta wote waliokaa Asia wakalisikia neno la Bwana, Wayahudi kwa Wayunani.

Mambo hayo yalipokwisha kumalizika, Paolo akaazimu rohoni mwake kupita kati ya Makedonia na Akaia aende Yerusalemi, akisema, Baada ya kuwako huko, yanipasa kuuona na Rumi.

na majadiliano ya watu walioharibiwa akili zao, walioikosa kweli, wakidhani ya kuwa utawa ni njia ya kupata faida; ujitenge na watu kama hao,

Twajua ya kuwa sisi tu wa Mungu; na dunia yote pia hukaa katika yule mwovu.

Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimejeruhi jeraha ya mauti. Pigo lake la mauti likaponywa, dunia yote ikastaajabu nyama ya nyama yule.

Watu wote wakaao juu ya inchi wakamsujudu, ambao majina yao hayakuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana kondoo aliyechinjwa kabla ya kuwekwa misingi ya dunia.

Malaika wa tatu akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu akimsujudu nyama na sanamu yake, na kupokea alama katika kipaji cha uso wake au katika mkono wake,

Tufuate:

Matangazo

Matangazo