Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 19:26 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

26 Tena mnaona na kusikia ya kwamba si katika Efeso tu, bali katika Asia yote pia, Paolo huyo amewaaminisha watu wengi na kuwageuza nia zao, akisema ya kwamba miungu inayofanywa kwa mikono siyo Mungu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 Sasa, mnaweza kusikia na kujionea wenyewe mambo Paulo anayofanya, si hapa Efeso tu, ila pia kote katika Asia. Yeye amewashawishi na kuwageuza watu wakakubali kwamba miungu ile iliyotengenezwa na watu si miungu hata kidogo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 Sasa, mnaweza kusikia na kujionea wenyewe mambo Paulo anayofanya, si hapa Efeso tu, ila pia kote katika Asia. Yeye amewashawishi na kuwageuza watu wakakubali kwamba miungu ile iliyotengenezwa na watu si miungu hata kidogo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 Sasa, mnaweza kusikia na kujionea wenyewe mambo Paulo anayofanya, si hapa Efeso tu, ila pia kote katika Asia. Yeye amewashawishi na kuwageuza watu wakakubali kwamba miungu ile iliyotengenezwa na watu si miungu hata kidogo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 Mnaona na kusikia jinsi huyu Paulo amewashawishi na kuwapoteza watu wengi hapa Efeso na karibu jimbo lote la Asia. Anasema kwamba miungu iliyofanywa kwa mikono ya wanadamu si miungu hata kidogo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 Pia ninyi mmeona na kusikia jinsi ambavyo si huku Efeso peke yake lakini ni karibu Asia yote, huyu Paulo amewashawishi na kuvuta idadi kubwa ya watu kwa kusema kuwa miungu iliyotengenezwa na watu si miungu.

Tazama sura Nakili




Matendo 19:26
23 Marejeleo ya Msalaba  

Sisi nasi tu wana Adamu hali moja na ninyi; twawakhubiri khabari njema mgenke na kuyaacha mambo haya ya ubatili na kumwelekea Mungu aliye hayi, aliyeumba mbingu na inchi na bahari na vitu vyotc vilivyomo:


Bassi, kwa kuwa sisi tu wazao wa Mungu, haitupasi kudhani ya kuwa Uungu ni mfano wa dhahabu au fedha au jiwe, vitu vilivyochongwa kwa ustadi na akili za wana Adamu.


Wakalika Efeso, akawaacha huko. Yeye mwenyewe akaingia katika sunagogi, akahujiana na Wayahudi.


IKAWA, Apollo alipokuwa Korintho, Paolo, akiisba kupita kati ya inchi za juu, akafika Efeso: akakutana na wanafunzi kadha wa kadba huko:


Mambo haya yakaendelea kwa muda wa miaka miwili, hatta wote waliokaa Asia wakalisikia neno la Bwana, Wayahudi kwa Wayunani.


Akawakusanya hao, pamoja na wengine wenye kazi ile ile, akasema, Enyi wanaume, mnajua ya kuwa utajiri wetu hutoka katika kazi hii.


Mwajua ya kuwa mlipokuwa Mataifa mlichukuliwa kwa sanamu zisizonena, kama mlivyoongozwa.


Bassi, kwa khabari ya kuvila vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu; twajua ya kuwa sanamu si kitu katika ulimwengu, na ya kuwa hapana Mungu mwingine illa mmoja tu.


Lakini wakati ule, kwa kuwa hamkujua Mungu, mliwatumikia wao ambao kwa asili si miungu.


Maana wao wenyewe wanatangaza khabari zetu, jinsi kulivyokuwa kuingia kwetu kwenu; na jinsi mlivyomgeukia Mungu, mkaziacha sanamu illi kumtumikia Mungu aliye hayi, wa kweli,


Na wana Adamu waliosalia, wasiouawa kwa mapigo hayo, hawakuzitubia kazi za mikono yao hatta wasiwasujudu mashetani, na sanamu za dhahabu na za fedha na za shaba na za mawe na za mili, zisizoweza kuona wala kusikia wala kuenenda.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo