Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 19:21 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

21 Mambo hayo yalipokwisha kumalizika, Paolo akaazimu rohoni mwake kupita kati ya Makedonia na Akaia aende Yerusalemi, akisema, Baada ya kuwako huko, yanipasa kuuona na Rumi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Baada ya mambo hayo, Paulo aliamua kwenda Yerusalemu kwa kupitia Makedonia na Akaya. Alisema, “Baada ya kufika huko, itanilazimu kuona Roma pia.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Baada ya mambo hayo, Paulo aliamua kwenda Yerusalemu kwa kupitia Makedonia na Akaya. Alisema, “Baada ya kufika huko, itanilazimu kuona Roma pia.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Baada ya mambo hayo, Paulo aliamua kwenda Yerusalemu kwa kupitia Makedonia na Akaya. Alisema, “Baada ya kufika huko, itanilazimu kuona Roma pia.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Baada ya mambo haya kutukia, Paulo akakusudia rohoni kwenda Yerusalemu kupitia Makedonia na Akaya. Akasema, “Baada ya kufika huko, yanipasa pia kwenda Rumi.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Baada ya mambo haya kutukia, Paulo akakusudia rohoni kwenda Yerusalemu kupitia Makedonia na Akaya. Akasema, “Baada ya kufika huko, yanipasa pia kwenda Rumi.”

Tazama sura Nakili




Matendo 19:21
31 Marejeleo ya Msalaba  

Siku ya pili tukafika Neapoli na kutoka hapo tukafika Filippi, mji wa Makedonia, mji ulio mkuu katika wilaya ile, nayo ni Kolonia ya Kirumi; tukawa katika mji huu, tukikaa siku kadha wa kadha.


Hatta Gallio alipokuwa Prokonsuli wa Akaya, Wayahudi wakamwendea Paolo kwa nia moja, wakamleta mbele ya kiti cha hukumu,


bali aliagana nao, akisema. Sina buddi kufanya siku kuu hii inayokuja Yerusalemi: lakini nitarejea kwenu, Mungu akinijalia.


Akatuma watu wawili miongoni mwa wale waliomkhudumia kwenda Makedonia, nao ni Timotheo na Erasto, yeye mwenyewe akakaa katika Asia kitambo.


Mji wote ukajaa ghasia, wakaenda mbio wakaingia theatro kwa moyo mmoja, wakiisha kuwakamata Gaio na Aristarko, watu wa Makedonia waliosafiri pamoja na Paolo.


Kwa sababu Paolo amekusudia kupita Efeso merikebuni, asije akakawia katika Asia: kwa maana alikuwa akifanya haraka, akitaka kuwahi Yerusalemi siku ya Pentekote, kama ikiwezekana.


Bassi, sasa angalieni, nashika njia kwenda Yerusalemi nimefungwa rohoni, nisijue mambo yatakayonikuta huko;


Tulipolika Yerusalemi ndugu wakatukaribisha kwa furaha.


Tukiisha kuwaona wanafunzi tukakaa huko siku saba, nao wakamwambia Paolo kwa uwezo wa Roho Mtakatifu asipande kwenda Yerusalemi.


Usiku ule Bwana akasimama karibu nae, akasema, Uwe na moyo mkuu, Paolo; kwa sababu, kama ulivyonishuhudia khabari zangu Yerusalemi, imekupasa kunishuhudia vivyo hivyo Rumi.


BASSI ilipoamriwa tusafiri hatta Italia, wakamtia Paolo na wafungwa wengine katika mikono ya akida mmoja, jina lake Yulio, wa kikosi cha Augusto.


Usiogope, Paolo, huna buddi kusimama mbele ya Kaisari: tena, tazama, Mungu amekupa watu wote wanaosafiri pamoja nawe.


Tulipoingia Rumi akida akawatia wafungwa katika mikono ya jemadari wa walinzi wa Praitorio: bali Paolo alipewa rukhusa kukaa kwake mwenyewe pamoja na askari aliyemlinda.


kwa maana ninatamani sana kuwaona, nipate kuwapeni karama ya rohoni, illi mfanywe imara;


Sipendi msiwe na khahari, ndugu zangu, ya kuwa marra nyingi nalikusudia kuja kwemi, nikazuiliwa hatta sasa, illi nipate kuwa na matunda kwenu ninyi pia kama nilivyo navyo katika mataifi mengine.


Kwa hiyo, kwa upande wangu, mimi ni tayari kuikhubiri Injili hatta na kwenu ninyi muaokaa Rumi;


Lakini nitakuja kwenu, nikipita kati ya Makedonia; maana napita kati ya Makedonia.


Lakini nitakuja kwemi upesi, Bwana akipenda, nami nitajua, si neno lao waliojivuna, bali nguvu zao.


na kupata ziada hatta kuikhuhiri Injili katika inchi zilizo mpaka mmoja na inchi zenu; tusijisifu katika cheo cha mtu mwingine kwa mambo yaliyokwisha kutengenezwa.


KIISHA, baada va miaka kumi na minane, nalipanda kwenda Yerusalemi pamoja na Barnaba, nikamchukua na Tito pamoja nami.


hatta mkawa mfano kwa watu wote waaminio katika Makedonia, na katika Akaya.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo