Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Matendo 19:19 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

19 Na watu wengi katika wale waliotumia mambo ya uganga wakakusanya vitabu vyao, wakavichoma moto mbele ya watu wote: wakafanya hesabu ya thamani yake wakaona ya kwamba yapata fedha khamsini elfu.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Wengine waliokuwa wameshughulikia mambo ya uchawi hapo awali, walikusanya vitabu vyao, wakavichoma mbele ya wote. Walikisia gharama ya vitabu hivyo, wakaona yafikia vipande 50,000 vya fedha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Wengine waliokuwa wameshughulikia mambo ya uchawi hapo awali, walikusanya vitabu vyao, wakavichoma mbele ya wote. Walikisia gharama ya vitabu hivyo, wakaona yafikia vipande 50,000 vya fedha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Wengine waliokuwa wameshughulikia mambo ya uchawi hapo awali, walikusanya vitabu vyao, wakavichoma mbele ya wote. Walikisia gharama ya vitabu hivyo, wakaona yafikia vipande 50,000 vya fedha.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Idadi kubwa ya wale waliofanya mambo ya uganga wakaleta vitabu vyao na kuviteketeza kwa moto hadharani. Walipofanya hesabu ya thamani ya vitabu vilivyoteketezwa ilikuwa drakma elfu hamsini za fedha.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Idadi kubwa ya wale waliofanya mambo ya uganga wakaleta vitabu vyao na kuviteketeza kwa moto hadharani. Walipofanya hesabu ya thamani ya vitabu vilivyoteketezwa ilikuwa drakma 50,000 za fedha.

Tazama sura Nakili

Matendo 19:19
23 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi, kadhalika killa mmoja wenu asiyeviacha vitu vyote alivyo navyo hawezi kuwa mwanafunzi wangu.

Ama mwanamke gani aliye na rupia kumi, akipotewa na rupia mmoja, asiyewasha taa, na kuifagia nyumba, akitatuta kwa bidii, hatta atakapoiona?

Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote cha Kupro, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa nwongo, Myahudi jina lake Bar-Yesu:

Lakini Eluma, yule mchawi (maana ndio tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali moyo wa kuiacha Imani.

Na wengi wa wale walioamini wakaja wakaungama, wakidhihirisha matendo yao.

Maana mliwaonea huruma wale waliokuwa katika mafungo, mkakubali kwa furaba kunyangʼauywa mali zenu, mkijua nafsini mwenu kwamba mna mali mbinguni iliyo njema zaidi, idumnyo.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo