Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Matendo 19:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 Na yule mtu aliyepagawa na pepo akawarukia, akawaweza, akawashinda, hatta wakatoka mbio katika nyumba ile uchi na wamejeruhi.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Kisha yule mtu aliyepagawa aliwarukia wote kwa kishindo, akawashinda nguvu. Na hao watoto wa Skewa wakakimbia kutoka ile nyumba wakiwa uchi na wamejaa majeraha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Kisha yule mtu aliyepagawa aliwarukia wote kwa kishindo, akawashinda nguvu. Na hao watoto wa Skewa wakakimbia kutoka ile nyumba wakiwa uchi na wamejaa majeraha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Kisha yule mtu aliyepagawa aliwarukia wote kwa kishindo, akawashinda nguvu. Na hao watoto wa Skewa wakakimbia kutoka ile nyumba wakiwa uchi na wamejaa majeraha.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Kisha yule mtu aliyekuwa na pepo mchafu akawarukia, akawashambulia vikali, akawashinda nguvu wote, wakatoka ndani ya ile nyumba wakikimbia wakiwa uchi na wenye majeraha.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Kisha yule mtu aliyekuwa na pepo mchafu akawarukia, akawashambulia vikali, akawashinda nguvu wote, wakatoka ndani ya ile nyumba wakikimbia wakiwa uchi na wenye majeraha.

Tazama sura Nakili

Matendo 19:16
8 Marejeleo ya Msalaba  

Wakamwendea Yesu, wakamwona yule mwenye pepo, ameketi, amevaa nguo, ana akili zake, nae ndiye aliyekuwa na ile legione; wakaogopa.

Kwa sababu amemwamuru yule pepo mchafu kumtoka mtu yule. Maana marra nyingi amempagaa, nae akafungwa, akilindwa, na kufungwa minyororo na pingu, akavikata vile vifungo, akafukuzwa na yule pepo hatta jangwani.

Wakatoka waone khabari iliyotokea. Wakamwendea Yesu, wakamwona yule mtu aliyetokwa na wale pepo ameketi migunni pa Yesu, amevaa nguo, ana akili zake: wakaogopa.

Yule pepo akawajibu, Yesu namjua na Paolo namfahamu, bali ninyi ni nani?

Khabari hii ikajulikana na Wayahudi wote na Wayunani waliokaa Efeso, khofu ikawaingia wote, jina la Bwana Yesu likaadhimishwa.

Akaondoka upesi akasimama, akaanza kwenda: akaingia ndani ya hekalu pamoja nao, akienda, akiruka, akimsifu Mungu.

wakiwaahidia uhuru, nao wenyewe ni watumwa wa uharibifu. Maana mtu akishindwa na mtu, huwa mtumwa wa mtu yule.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo