Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 18:8 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

8 Na Krispo, mkuu wa sunagogi, akamwamini Bwana pamoja na nyumba yake yote. Wakorintho wengi wakasikia, wakaamini, wakabatizwa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Krispo, mkuu wa hilo sunagogi, alimwamini Bwana yeye pamoja na jamaa yake yote. Wakorintho wengi waliusikiliza ujumbe huo, wakaamini na kubatizwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Krispo, mkuu wa hilo sunagogi, alimwamini Bwana yeye pamoja na jamaa yake yote. Wakorintho wengi waliusikiliza ujumbe huo, wakaamini na kubatizwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Krispo, mkuu wa hilo sunagogi, alimwamini Bwana yeye pamoja na jamaa yake yote. Wakorintho wengi waliusikiliza ujumbe huo, wakaamini na kubatizwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Kiongozi wa hilo sinagogi, aliyeitwa Krispo, akamwamini Bwana, yeye pamoja na watu wote wa nyumbani mwake. Nao Wakorintho wengi waliomsikia Paulo pia wakaamini na kubatizwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Kiongozi wa hilo sinagogi, aliyeitwa Krispo, akamwamini Bwana Isa, yeye pamoja na watu wote wa nyumbani mwake. Nao Wakorintho wengi waliomsikia Paulo pia wakaamini na kubatizwa.

Tazama sura Nakili




Matendo 18:8
25 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi, enendeni, kawafanyeni mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;


Kumbe! akaja mtu mmoja katika wakuu wa sunagogi, jina lake Yairo: hatta alipomwona, akaanguka miguuni pake,


Hatta alipokuwa akisema wakaja watu kutoka kwa mkuu wa sunagogi, wakinena, Binti yako amekwisha kufa: ya nini kuzidi kumsumbua mwalimu?


mtu nitawa, mcha Mungu, yeye na nyumba yake yote, nae alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu siku zote.


atakaekuambia maneno ambayo utaokolewa nayo, wewe na nyumba yako yote.


Kiisha baada ya kusomwa torati na chuo cha manabii, wakuu wa sunagogi wakatuma mtu kwao, na kuwaambia, Ndugu, kama mkiwa na neno la kuwafaa watu hawa, lisemeni.


Akawaleta juu nyumbani kwake, akawaandalia, akafurahi sana, yeye na nyumba yake yote, maana amekwisha kumwamini Mungu.


BAADA ya mambo haya Paolo akatoka Athene akalika Korintho.


Na Wayunani wote wakamshika Sosthene, mkuu wa sunagogi, wakampiga mbele ya kiti cha hukumu. Na Gallio hakuyaona mambo hayo kuwa kitu.


IKAWA, Apollo alipokuwa Korintho, Paolo, akiisba kupita kati ya inchi za juu, akafika Efeso: akakutana na wanafunzi kadha wa kadba huko:


Lakini walimpomwamini Filipo, akizikhubiri khabari njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake.


kwa kanisa la Mungu lililo katika Korintho, lililotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu pamoja na wote wanaoliitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo killa mahali, Bwana wao na wetu:


PAOLO, mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu, na Timothieo ndugu yetu, kwa kanisa la Mungu lililo katika Korintho, pamoja na watakatifu wote walio katika inchi yote ya Akaia:


Lakini mimi namwitia Mungu awe shahidi juu ya roho yangu, ya kwamba, kwa kuwahurumia sijaenda Korintho.


Vinywa vyetu vimewafunukia ninyi, enyi Wakorintho; mioyo yetu imekunjuliwa.


Trofimo nalimwacha Mileto, hawezi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo