Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 18:6 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

6 Walipopingamana nae na kutukana, akakungʼuta mavazi yake, akawaambia, Damu yenu na iwe juu ya vichwa vyenu: mimi ni safi: langu sasa nitakwenda kwa watu wa mataifa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Walipompinga na kuanza kumtukana, aliyakunguta mavazi yake mbele yao akisema, “Mkipotea ni shauri lenu wenyewe; mimi sina lawama yoyote juu ya jambo hilo. Na tangu sasa nitawaendea watu na mataifa mengine.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Walipompinga na kuanza kumtukana, aliyakunguta mavazi yake mbele yao akisema, “Mkipotea ni shauri lenu wenyewe; mimi sina lawama yoyote juu ya jambo hilo. Na tangu sasa nitawaendea watu na mataifa mengine.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Walipompinga na kuanza kumtukana, aliyakung'uta mavazi yake mbele yao akisema, “Mkipotea ni shauri lenu wenyewe; mimi sina lawama yoyote juu ya jambo hilo. Na tangu sasa nitawaendea watu na mataifa mengine.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Wayahudi walipompinga Paulo na kukufuru, yeye aliyakung’uta mavazi yake, akawaambia, “Damu yenu na iwe juu ya vichwa vyenu! Mimi sina hatia, nimetimiza wajibu wangu. Kuanzia sasa nitawaendea watu wa Mataifa.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Wayahudi walipompinga Paulo na kukufuru, yeye aliyakung’uta mavazi yake, akawaambia, “Damu yenu na iwe juu ya vichwa vyenu! Mimi sina hatia, nimetimiza wajibu wangu. Kuanzia sasa nitawaendea watu wa Mataifa.”

Tazama sura Nakili




Matendo 18:6
37 Marejeleo ya Msalaba  

Na mtu asipowakaribisha wala kuyasikiliza maneno yenu, mtokapo katika nyumba ile, au mji ule, kungʼuteni mavumbi ya miguuni mwenu.


Wakamwambia, Atawaangamiza wabaya wale; nae atawapangisha mizabibu wakulima wengine, watakaomlipa matunda kwa wakati wake.


Kwa sababu hii nawaambieni, ya kwamba ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, na watapewa taifa lingine wenye kuzaa matunda yake.


Watumishi wale wakatoka wakaingia njia kuu, wakakusanya wote waliowaona, waovu na wema: arusi ikajaa wageni.


Watu wote wakajibu wakasema, Damu yake na iwe juu yetu, na juu ya watoto wetu.


Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magbaribi, wataketi pamoja na Ibrabimu, na Isaak, na Yakob katika ufalme wa mbinguni;


Wakamnena na mengine mengi kwa kufuru.


Na wo wote wasiowakarihisheni, mtokapo katika mji ule, yakungʼuteni mavumbi ya miguuni mwenu illi kuwa ushuhuda juu yao.


Nao wakawakungʼutia mavumbi ya miguu yao, wakaenda Ikonio.


Na marra nyingi katika masunagogi mengi naliwaadhibu, nikawashurutisha kukufuru; nikawaonea hasira kama nina wazimu, nikawaudhi hatta katika miji ya ugenini.


hali kwanza niliwakhubiri wale wa Dameski na Yerusalemi, na katika inchi yote ya Yahudi, na watu wa mataifa, watubu wakamwelekee Mungu, wakiyatenda matendo yanayopatana na kutubu kwao.


Bassi ijulikane kwenu ya kwamba wokofu huu wa Mungu umepelekwa kwa mataifa, nao watasikia.


Au Mungu ni Mungu wa Wayahudi tu? Siye Mungu wa mataifa pia? Naam, wa mataifa pia;


Usimwekee mtu mikono kwa haraka, wala usishiriki dhambi za watu wengine.


akiwaonya kwai npole washindanao nae, illi, kama ikiwezekana, Mungu awape kutubu na ujuzi wa kweli,


Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni kheri yenu, kwa kuwa Roho ya utukufu na ya Mungu unawakalia; kwa hawo anatukanwa, bali kwenu ninyi anatukuzwa.


mambo ambayo wao huona kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao hatta ufisadi usio kiasi, wakiwatukaneni;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo