Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 18:4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

4 Akatoa hoja zake katika sunagogi killa sabato akawavuta Wayahudi na Wayunani waamini.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Kila Sabato alifanya majadiliano katika sunagogi akijaribu kuwavuta Wayahudi na Wagiriki.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Kila Sabato alifanya majadiliano katika sunagogi akijaribu kuwavuta Wayahudi na Wagiriki.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Kila Sabato alifanya majadiliano katika sunagogi akijaribu kuwavuta Wayahudi na Wagiriki.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Kila Sabato Paulo alikuwa akihojiana nao katika sinagogi, akijitahidi kuwashawishi Wayahudi na Wayunani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Kila Sabato Paulo alikuwa akihojiana nao katika sinagogi, akijitahidi kuwashawishi Wayahudi na Wayunani.

Tazama sura Nakili




Matendo 18:4
18 Marejeleo ya Msalaba  

Akamwambia, Wasiposikia Musa na manabii, ajapoondoka mtu katika wafu, hawatashawishwa.


Akaenda Nazareti, mahali alipokuwa amelelewa: akaingia katika sunagogi siku ya sabato, kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama illi asome.


Bassi Wayahudi wakasemezana wao kwa wao, Huyu atakwenda wapi hatta sisi tusimwone? Atakwenda kwa Utawauyiko wa Wayunani na kuwafundisha Wayunani?


Lakini wao wakatoka Perga, wakapita kati ya inchi, wakafika Antiokia mji wa Pisidia, wakaingia katika sunagogi siku ya sabato, wakaketi.


IKAWA huko Ikonio wakaingia pamoja katika sunagogi ia Wayahudi, wakanena; hatta jamaa kubwa ya Wayahudi na ya Wayunani wakaamini.


Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thessaloniki, kwa kuwa walilipokea Neno kwa uelekefu wa moyo, wakayachunguza maandiko, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo.


Bassi katika sunagogi akahujiana na Wayahudi nao waliomcha Mungu, na killa siku sokoni na wale waliokutana nae.


wakisema, Mtu huyu huwavuta watu illi wamwabudu Mungu kinyume cha sharia yetu.


Wakalika Efeso, akawaacha huko. Yeye mwenyewe akaingia katika sunagogi, akahujiana na Wayahudi.


Tena mnaona na kusikia ya kwamba si katika Efeso tu, bali katika Asia yote pia, Paolo huyo amewaaminisha watu wengi na kuwageuza nia zao, akisema ya kwamba miungu inayofanywa kwa mikono siyo Mungu.


Akaingia ndani ya sunagogi, akanena kwa ujasiri, akihujiana na watu kwa muda wa miezi mitatu, na kuwavuta waamini mambo ya ufalme wa Mungu.


Agrippa akamwambia Paolo, Kwa maneno machache wataka kunifanya kuwa Mkristo.


Wakiislia kuwekana kwa siku, wakaja kwake nyumbani kwake, watu wengi sana, akawaeleza kwa taratibu na kuushuhudia ufalme wa Mungu, akiwaonya mambo yake Yesu, kwa maneno ya sharia ya Musa na ya manabii, tangu assubuhi hatta jioni.


Marra akamkhubiri Yesu katika masunagogi, kwamba yeye ni Mwana wa Mungu.


Bassi tukiijua khofu ya Bwana, twawavuta wana Adamu; lakini tumedhihirishwa mbele za Mungu. Nami natumaini ya kuwa tunadhihirishwa katika dhamiri zenu pia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo