Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 18:25 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

25 Mtu huyu alikuwa amefundishwa njia ya Bwana; na kwa kuwa roho yake ilikuwa ikiwaka, alianza kunena na kufundisha kwa usahihi khabari za Bwana; nae alijua ubatizo wa Yohana tu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

25 Alikuwa amefundishwa juu ya hiyo njia ya Bwana, na akiwa motomoto, aliongea juu ya habari za Yesu akafundisha kwa usahihi ingawa alikuwa amepata ubatizo wa Yohane tu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

25 Alikuwa amefundishwa juu ya hiyo njia ya Bwana, na akiwa motomoto, aliongea juu ya habari za Yesu akafundisha kwa usahihi ingawa alikuwa amepata ubatizo wa Yohane tu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

25 Alikuwa amefundishwa juu ya hiyo njia ya Bwana, na akiwa motomoto, aliongea juu ya habari za Yesu akafundisha kwa usahihi ingawa alikuwa amepata ubatizo wa Yohane tu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

25 Alikuwa amefundishwa katika njia ya Bwana Isa, naye alikuwa na bidii katika roho, akafundisha kwa usahihi kuhusu Isa, ingawa alijua tu ubatizo wa Yahya.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

25 Alikuwa amefundishwa katika njia ya Bwana Isa, naye alikuwa na bidii katika roho, akafundisha kwa usahihi juu ya Isa, ingawa alijua tu ubatizo wa Yahya.

Tazama sura Nakili




Matendo 18:25
27 Marejeleo ya Msalaba  

Sauti yake aliae jangwani, Itengenezeni njia ya Bwana, Nyosheni mapito yake.


Hatta walipofika wakamwambia, Mwalimu, twajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli, wala hujali cheo cha mtu; kwa maana hutazami sura za watu: lakini katika kweli waifundisha njia ya Mungu. Je! ni halali kumpa Kaisari kodi au sivyo? Tumpe, tusimpe?


upate kujua usahihi wa maneno yale uliyofundishwa.


Watu wote na watoza ushuru waliposikia wakampa Mungu haki, kwa kuwa wamebatizwa kwa ubatizo wa Yohana.


Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa shetani, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka?


Akamfuata Paolo na sisi, akipiga kelele, akisema, Watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu, wenye kutukhubiri njia ya wokofu.


Akaanza kunena bila khofu katika sunagogi: hatta Akula na Priskilla walipomsikia wakamchukua kwao, wakamweleza njia ya Bwana kwa usahihi zaidi.


Hatta wakati huo kukatukia ghasia si haba katika khabari ya Njia ile.


Akawauliza, Bassi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, Kwa ubatizo wa Yohana.


Lakini wengine walikaidi, wakakataa kuamini, wakiitukana ile Njia mbele ya mkutano; bassi, akaondoka akawaacha, akawatenga wanafunzi nao, akahujiana na watu killa siku katika darasa ya mtu mmoja, jina lake Tyranno.


akataka ampe khati za kwenda Dameski zilizoandikwa kwa masunagogi, illi akiona watu wa Njia hii, waume kwa wake, awafunge na kuwaleta Yerusalemi.


kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana;


Hakuna mfanya vita ajitiae katika shughuli za dunia; illi ampendeze yeye aliyemwandika awe askari.


Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo