Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 18:24 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

24 Bassi Myahudi mmoja, jina lake Apollo, mzalia wa Iskanderia, mtu wa elimu, akalika Efeso; nae alikuwa hodari wa maandiko.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 Myahudi mmoja aitwaye Apolo, mzaliwa wa Aleksandria, alifika Efeso. Alikuwa mtu mwenye ufasaha wa kuongea na mwenye ujuzi mkubwa wa Maandiko Matakatifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 Myahudi mmoja aitwaye Apolo, mzaliwa wa Aleksandria, alifika Efeso. Alikuwa mtu mwenye ufasaha wa kuongea na mwenye ujuzi mkubwa wa Maandiko Matakatifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 Myahudi mmoja aitwaye Apolo, mzaliwa wa Aleksandria, alifika Efeso. Alikuwa mtu mwenye ufasaha wa kuongea na mwenye ujuzi mkubwa wa Maandiko Matakatifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 Basi akaja Efeso Myahudi aliyeitwa Apolo, mzawa wa Iskanderia. Alikuwa na elimu kubwa, pia alikuwa na ujuzi wa Maandiko.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 Basi akaja Efeso Myahudi mmoja, jina lake Apolo, mwenyeji wa Iskanderia. Yeye alikuwa na elimu kubwa, pia alikuwa hodari katika Maandiko.

Tazama sura Nakili




Matendo 18:24
22 Marejeleo ya Msalaba  

Akawaambia, Kwa sababu hii, killa mwandishi mwenye elimu ya ufalme wa mbinguni amefanana na mtu mwenye nyumba atoae katika hazina yake vitu vipya na vya kale.


Akawaambia, Mambo gani? Wakamwambia, Mambo ya Yesu Mnazareti, aliyekuwa mtu nabii mwenye nguvu kwa tendo na kwa neno mbele za Mungu na watu wote;


Wakalika Efeso, akawaacha huko. Yeye mwenyewe akaingia katika sunagogi, akahujiana na Wayahudi.


bali aliagana nao, akisema. Sina buddi kufanya siku kuu hii inayokuja Yerusalemi: lakini nitarejea kwenu, Mungu akinijalia.


Kwa maana aliwashinda Wayahudi kabisa kabisa mbele ya watu wote, akiwaonyesha kwa maneno ya maandiko ya kuwa Yesu ni Kristo.


IKAWA, Apollo alipokuwa Korintho, Paolo, akiisba kupita kati ya inchi za juu, akafika Efeso: akakutana na wanafunzi kadha wa kadba huko:


Na huko yule akida akakuta merikebu ya Iskanderia, tayari kusafiri hatta Italia, akatupandisha.


Lakini baadhi ya watu wa sunagogi lililokwitwa sunagogi la Malibertino, na la Wakurene na la Waiskanderia, na la wale wa Kilikia na Asia, wakaondoka wakajadiliana na Stefano:


Musa akafundishwa hekima yote ya Misri, akawa hodari wa maneno na matendo.


Bassi, nasema neno hili, ya kwamba killa mtu wa kwenu husema, Mimi wa Paolo, na mimi wa Apollo, na mimi wa Kefa, na mimi wa Kristo.


Lakini kwa khabari za Apollo, ndugu yetu, nalimsihi sana aende kwenu pamoja nao ndugu, nae hakupenda kabisa kwenda sasa; lakini atakwenda sitakupopata nafasi.


Mambo haya, ndugu, nimeyafanya kuwa mfano wa mimi na wa Apollo kwa ajili yemi, illi kwa khabari zetu mpate kujifunza katika fikara zenu kutokuruka mpaka wa yale yaliyoandikwa; mtu mmoja asijivune juu ya mwenziwe, kwa ajili ya mtu mwingine.


Maana wasema, Nyaraka zake nzito, hodari; bali akiwapo mwenyewe mwilini yu dhaifu, na maneno yake hayawi kitu.


Neno la Kristo likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; kwa neema mkimwimbia Bwana mioyoni mwenu.


Zena, mjua sharia, na Apollo uwusafirishe kwa bidii; wasipungukiwe cho chote.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo