Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 18:23 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

23 Hatta akiisha kukaa huko siku kadha wa kadha akaondoka, akapita kati ya inchi ya Galatia na Frugia, mji kwa mji, akiwatia moyo wanafunzi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Alikaa huko muda mfupi, halafu akaendelea na safari kwa kupitia sehemu za Galatia na Frugia akiwatia moyo wafuasi wote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Alikaa huko muda mfupi, halafu akaendelea na safari kwa kupitia sehemu za Galatia na Frugia akiwatia moyo wafuasi wote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Alikaa huko muda mfupi, halafu akaendelea na safari kwa kupitia sehemu za Galatia na Frugia akiwatia moyo wafuasi wote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Baada ya kukaa huko kwa muda, akaondoka na kwenda sehemu moja hadi nyingine huko Galatia na Frigia, akiwaimarisha wanafunzi wote.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Baada ya kukaa huko kwa muda, akaondoka na kwenda sehemu moja hadi nyingine huko Galatia na Frigia, akiwaimarisha wanafunzi wote.

Tazama sura Nakili




Matendo 18:23
22 Marejeleo ya Msalaba  

nimeona vema na mimi, nikiisha kujipatia khabari zilizo sahihi za mambo yote tokea awali, kukuandikia kwa taratibu. Theofilo il-aziz:


lakini nimekuombea, illi imani yako isipunguke; nawe uongokapo, wathubutishe ndugu zako.


Akamtokea malaika toka mbinguni akimtia nguvu.


wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya shidda nyingi.


Tena Yuda na Sila, kwa kuwa wao wenyewe ni manabii, wakawausia ndugu kwa maneno mengi, wakawathubutisha.


Akapita katika Shami na Kilikia akawatia moyo makanisa.


Nao wakatoka gerezani wakaingia nyumbani mwa Ludia; na walipokwisha kuwaona ndugu wakawafariji, wakaenda zao.


Wakapita katika inchi ya Frugia na Galatia, wakakatazwa na Roho Mtakatifu, wasilikhubiri Neno katika Asia.


IKAWA, Apollo alipokuwa Korintho, Paolo, akiisba kupita kati ya inchi za juu, akafika Efeso: akakutana na wanafunzi kadha wa kadba huko:


Frugia na Pamfulia, Misri na pande za Libua karibu na Kurene, na Warumi wageni, Wayahudi na Waongofu,


KWA khabari ya ile changizo kwa ajili ya watakatifu, kama vile nilivyoamuru makanisaya Galatia, na ninyi fanyeni vivyo hivyo.


na ndugu wote walio pamoja nami, kwa makanisa ya Galatia,


Kama tulivyotangulia kusema, na sasa nasema tena, mtu awae yote akiwakhubiri injili illa hiyo tuliyowakhubiri, na alaaniwe.


na jaribu lililowapata katika mwili wangu hamkulidharau wala kulikataa, bali mlinipokea kama malaika wa Mungu, kama Yesu Kristo.


tukamtuma Timotheo ndugu yetu, mtumishi wa Mungu, mfanya kazi pamoja naswi katika Injili ya Kristo, kuwafanya ninyi imara na kuwafariji kwa ajili ya imani yenu,


Bassi, farijianeni kwa maneno haya.


Twawasihi, ndugu, waonyeni wale wasiokaa kwa taratihu, watieni moyo walio dhaifu, watieni nguvu wanyonge, vumilieni na watu wote.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo