Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 18:19 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

19 Wakalika Efeso, akawaacha huko. Yeye mwenyewe akaingia katika sunagogi, akahujiana na Wayahudi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Walifika Efeso na hapo Paulo aliwaacha Priskila na Akula, akaenda katika sunagogi, akajadiliana na Wayahudi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Walifika Efeso na hapo Paulo aliwaacha Priskila na Akula, akaenda katika sunagogi, akajadiliana na Wayahudi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Walifika Efeso na hapo Paulo aliwaacha Priskila na Akula, akaenda katika sunagogi, akajadiliana na Wayahudi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Walipofika Efeso, Paulo aliwaacha Prisila na Akila huko, lakini yeye akaingia kwenye sinagogi akawa anajadiliana na Wayahudi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Walipofika Efeso, Paulo aliwaacha Prisila na Akila huko, lakini yeye akaingia kwenye sinagogi akawa anajadiliana na Wayahudi.

Tazama sura Nakili




Matendo 18:19
21 Marejeleo ya Msalaba  

Walipotaka akae wakati mwingi zaidi, hakukubali:


bali aliagana nao, akisema. Sina buddi kufanya siku kuu hii inayokuja Yerusalemi: lakini nitarejea kwenu, Mungu akinijalia.


Bassi Myahudi mmoja, jina lake Apollo, mzalia wa Iskanderia, mtu wa elimu, akalika Efeso; nae alikuwa hodari wa maandiko.


Akatoa hoja zake katika sunagogi killa sabato akawavuta Wayahudi na Wayunani waamini.


IKAWA, Apollo alipokuwa Korintho, Paolo, akiisba kupita kati ya inchi za juu, akafika Efeso: akakutana na wanafunzi kadha wa kadba huko:


Khabari hii ikajulikana na Wayahudi wote na Wayunani waliokaa Efeso, khofu ikawaingia wote, jina la Bwana Yesu likaadhimishwa.


Tena mnaona na kusikia ya kwamba si katika Efeso tu, bali katika Asia yote pia, Paolo huyo amewaaminisha watu wengi na kuwageuza nia zao, akisema ya kwamba miungu inayofanywa kwa mikono siyo Mungu.


Waliposikia haya wakajaa hasira, wakapiga kelele, wakisema, Artemi wa Waefeso m mkuu.


Na karani wa mji alipokwisha kuwatuliza watu, akasema, Enyi wanaume wa Efeso, ni mtu gani asiyejua ya kuwa mji wa Efeso ni mtunzaji wa hekalu ya Artemi, mungu mke aliye mkuu, na wa kitu kile kilichoanguka kutoka mbinguni?


Kwa sababu Paolo amekusudia kupita Efeso merikebuni, asije akakawia katika Asia: kwa maana alikuwa akifanya haraka, akitaka kuwahi Yerusalemi siku ya Pentekote, kama ikiwezekana.


Toka Mileto Faolo akatuma watu kwenda hatta Efeso, akawaita wazee wa Kanisa.


Kwa maana wamemwona Trofimo Mwefeso, pamoja nae mjini, wakadhani ya kuwa Paolo amemwingiza katika hekalu.


Ikiwa, kwa jinsi ya kibinadamu, nalipigana na nyama wakali kule Efeso, nina faida gani wasipofufuka wafu? Tule, tukanywe, maana kesho tutakufa.


Lakini nitakaa katika Efeso mpaka Pentekote;


PAOLO, mtume wa Yesu Kristo, kwa mapenzi ya Mungu, kwa watakatifu walio katika Efeso na wanaomwamini Kristo Yesu;


Kama vile nilivyotaka ukae katika Efeso nilipokuwa nikisafiri kwenda Makedonia, illi, nwaagize wengine wasifundishe elimu ya namna nyingine,


Bwana na ampe kuona rehema kwa Bwana siku ile. Na jinsi alivyonikhudumia katika Efeso, wewe wajua sana.


Lakini Tukiko nalimpeleka Efeso.


ikinena, Mimi ni Alfa na Omega, wa kwanza na wa mwisho. Haya uonayo yaandike katika chuo, ukayapeleke kwa makanisa saba yaliyo katika Asia; Efeso, na Smurna, na Pergamo, na Thuatera, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia.


KWA malaika wa kanisa lililo katika Efeso andika; Haya ayanena yeye azishikae nyota saba katika mkono wake wa kuume, aendae kati kati ya vile vinara saba vya dhahabu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo