Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 18:18 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

18 Paolo akazidi kukaa huko siku nyingi, kiisha akaagana na ndugu akatweka kwenda Shami; na Priskilla na Akula wakaenda pamoja nae, alipokwisha kunyoa kichwa chake katika Kenkrea; maana alikuwa ana nadhiri.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Paulo alikaa bado na wale ndugu huko Korintho kwa siku nyingi. Kisha aliwaaga, akapanda meli kwenda Siria pamoja na Priskila na Akula. Huko Kenkrea, alinyoa nywele zake kwa sababu ya nadhiri aliyokuwa ameweka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Paulo alikaa bado na wale ndugu huko Korintho kwa siku nyingi. Kisha aliwaaga, akapanda meli kwenda Siria pamoja na Priskila na Akula. Huko Kenkrea, alinyoa nywele zake kwa sababu ya nadhiri aliyokuwa ameweka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Paulo alikaa bado na wale ndugu huko Korintho kwa siku nyingi. Kisha aliwaaga, akapanda meli kwenda Siria pamoja na Priskila na Akula. Huko Kenkrea, alinyoa nywele zake kwa sababu ya nadhiri aliyokuwa ameweka.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Baada ya kukaa Korintho kwa muda, Paulo akaagana na ndugu, akasafiri kwa meli kwenda Siria akiwa amefuatana na Prisila na Akila. Walipofika Kenkrea, Paulo alinyoa nywele zake kwa kuwa alikuwa ameweka nadhiri.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Baada ya kukaa Korintho kwa muda, Paulo akaagana na wale ndugu walioamini, akasafiri kwa njia ya bahari kwenda Shamu akiwa amefuatana na Prisila na Akila. Walipofika Kenkrea, Paulo alinyoa nywele zake kwa kuwa alikuwa ameweka nadhiri.

Tazama sura Nakili




Matendo 18:18
17 Marejeleo ya Msalaba  

Khabari zake zikaenea katika Sham yote; wakamletea watu waliokuwa hawawezi, walioshikwa mi maradhi mbali mbali na mateso, nao wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya.


Hatta alipokwisha kuagana nao akaenda zake mlimani kusali.


Siku zile akasimama Petro kati ya wanafunzi, akasema (jumla ya majina ilipata mia na ishirini),


Wakaandika hivi kwa mikono yao, Mitume na wazee na ndugu, kwa ndugu zetu walioko Antiokia na Shami na Kilikia, walio wa mataifa, salamu.


Akapita katika Shami na Kilikia akawatia moyo makanisa.


Akamwona Myahudi mmoja, jina lake Akula, mzalia wa Ponto; nae amekuja kutoka inchi ya italia siku za karibu, pamoja na Priskilla mkewe, kwa sababu Klaudio amewaamuru Wayahudi wote watoke Rumi.


Akaanza kunena bila khofu katika sunagogi: hatta Akula na Priskilla walipomsikia wakamchukua kwao, wakamweleza njia ya Bwana kwa usahihi zaidi.


Na alipotaka kuvuka bahari aende hatta Akaya, ndugu wakamhimiza, wakamwandikia barua kwa wanafunzi wale wamkaribishe; nae alipofika akawasaidia sana wale waliokwisha kuamini kwa neema ya Mungu.


Bassi fanya neno hili tunalokuambia: Wako kwetu watu wane waliofungwa na nadhiri.


Chukua watu hao, ujitakase pamoja nao, na kuwagharimia illi wanyoe vichwa vyao, watu wote wapate kujua ya kuwa khabari zile walizoambiwa juu yako si kitu, bali wewe mwenyewe unaenenda vizuri na kuishika sharia.


Na tulipoona Kupro tukaiacha upande wa kushoto: tukasafiri hatta Shami tukashuka Turo. Kwa maana huko ndiko marikebu yetu itakakoshusha shehena yake.


NAWAPENI sifa njema za Foibe ndugu yetu, aliye mwenye khuduma katika kanisa lilioko Kenkrea,


Nalikuwa Myahudi kwa Wayahudi, illi niwapate Wayahudi; kwa wale walio chini ya sharia, nalikuwa kama chini ya sharia, illi niwapate walio chini ya sharia.


Khalafu nalikwenda pande za Sham na Kilikia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo