Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 17:6 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

6 na wasipowakuta, wakamkokota Yason na baadhi ya ndugu mbele ya wakubwa wa mji, wakipiga kelele, wakisema, Watu hawa walioupindua ulimwengu wamefika na huku,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Lakini hawakuwapata na hivyo walimburuta Yasoni pamoja na ndugu wengine mpaka kwa wakuu wa mji, wakapiga kelele: “Watu hawa wamekuwa wakivuruga dunia yote na sasa wako hapa mjini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Lakini hawakuwapata na hivyo walimburuta Yasoni pamoja na ndugu wengine mpaka kwa wakuu wa mji, wakapiga kelele: “Watu hawa wamekuwa wakivuruga dunia yote na sasa wako hapa mjini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Lakini hawakuwapata na hivyo walimburuta Yasoni pamoja na ndugu wengine mpaka kwa wakuu wa mji, wakapiga kelele: “Watu hawa wamekuwa wakivuruga dunia yote na sasa wako hapa mjini.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Lakini walipowakosa wakamburuta Yasoni na ndugu wengine mbele ya maafisa wa mji, wakipaza sauti na kusema: “Watu hawa walioupindua ulimwengu wamekuja huku,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Lakini walipowakosa wakamburuta Yasoni na ndugu wengine mbele ya maafisa wa mji, wakipiga kelele: “Watu hawa ni wale walioupindua ulimwengu wamekuja huku,

Tazama sura Nakili




Matendo 17:6
18 Marejeleo ya Msalaba  

Na injili hii ya ufalme itakhubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; ndipo ule mwisho utakapokuja.


Nao wakamshurutisha, wakisema, Awataharakisha watu, akifundisha katika Yahudi yote, akianzia Galilaya hatta hapa.


Siku zile akasimama Petro kati ya wanafunzi, akasema (jumla ya majina ilipata mia na ishirini),


Marra ndugu wakawapeleka Paolo na Sila usiku hatta Beroya. Walipofika huko wakaingia katika sunagogi la Wayahudi.


Marra hiyo wale ndugu wakampeleka Paolo aende zake kana kwamba anakwenda njia ya pwani; bali Sila na Timotheo wakashinda huko.


Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa ujumbe wa mtu yule aliyemchagua; nae amewapa watu wote bayana ya mambo haya kwa kumfufua katika wafu.


Na Wayahudi wasioamini wakaona wivu, wakajitwalia watu kadha wa kadha katika watu ovyo wasio na sifa njema wakakutanisha mkutano, wakafanya ghasia mjini, wakawaendea watu wa nyumba ya Yason wakataka kuwapeleka mbele ya watu wa mji;


Kwa maana tamemwona mtu huyu mkorofi, muanzishaji wa fitina katika Mayahudi waliomo duniani, tena ni kichwa cha uzushi wa Wanazorayo.


Lakini tunataka kusikia kwako uonavyo wewe; kwa maana katika khabari za madhehebu hiyo tumekwisha kujua kwamba inanenwa vibaya kilia mahali.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo