Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 17:32 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

32 Bassi waliposikia khabari za ufufuo wa wafu wengine wakadhihaki: wengine wakasema, Tutakusikiliza tena khabari hiyo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

32 Walipomsikia Paulo anasema juu ya jambo la kufufuka kwa wafu, wengine wao waliangua kicheko; lakini wengine walisema, “Tunataka kukusikia tena juu ya jambo hili!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

32 Walipomsikia Paulo anasema juu ya jambo la kufufuka kwa wafu, wengine wao waliangua kicheko; lakini wengine walisema, “Tunataka kukusikia tena juu ya jambo hili!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

32 Walipomsikia Paulo anasema juu ya jambo la kufufuka kwa wafu, wengine wao waliangua kicheko; lakini wengine walisema, “Tunataka kukusikia tena juu ya jambo hili!”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

32 Waliposikia habari za ufufuo wa wafu, baadhi yao wakadhihaki, lakini wengine wakasema, “Tunataka kukusikia tena ukizungumza juu ya jambo hili.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

32 Waliposikia habari za ufufuo wa wafu, baadhi yao wakadhihaki, lakini wengine wakasema, “Tunataka kukusikia tena ukizungumza juu ya jambo hili.”

Tazama sura Nakili




Matendo 17:32
23 Marejeleo ya Msalaba  

Wakaanza kutoa udhuru, wote pia kwa nia moja. Wa kwanza akamwambia, Nimenunua shamba, sina buddi kwenda na kulitazama; nakuomba, unisamehe.


Na wale watu waliomshika Yesu, wakamdhihaki, wakampiga.


Bassi Herode akamtweza pamoja na askari zake akamdhihaki, akamvika mavazi mazurimazuri, akamrudisha kwa Pilato.


Askari wakamdhihaki, wakimjia, wakimpa siki, na kusema,


Tazameni, enyi mnaodharau, kjitaajabuni, katowekeni; kwa kuwa natenda kazi mimi siku zenu, kazi msiyoisadiki kabisa, ijapo mtu akiwasimulia sana.


Na baadhi ya Waepikurio na Wastoiko, matilosofo, wakakutana nae. Wengine wakasema, Mtu huyu mwenye maneno mengi anataka kusema nini? Wengine walisema, Anaonekana kuwa mtangaza khabari za miungu migeni, kwa maana alikuwa akikhubiri khabari za Yesu na ufufuo.


Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa ujumbe wa mtu yule aliyemchagua; nae amewapa watu wote bayana ya mambo haya kwa kumfufua katika wafu.


Bassi Paolo akaondoka akawaacha.


Wengine walidhihaki, wakisema, Wamelewa kwa mvinyo mpya.


Na Paolo alipokuwa akitoa hoja zake katika khabari ya haki na kiasi na hukumu itakayokuja, Feliki akafanya khofu akajihu, Sasa enenda zako, nami nikipata wasaa nitakuita tena.


hali walikuwa na maswali juu yake katika dini yao wenyewe, na katika khabari ya mtu mmoja Yesu, aliyekuwa amekwisha kufa, ambae Paolo alishika kusema kwamba yu hayi.


Kwa nini limedhaniwa nanyi kuwa neno lisilosadikika, kwamba Mungu awafufua wafu?


bali sisi tunamkhubiri Kristo, aliyesulibiwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni upumbavu,


Bassi, ikiwa Kristo amekhubiriwa kwenu ya kwamba amefufuka, mbona wengine wenu wasema kwamba hakuna kiyama ya wafu?


Sisi tu wapumbavu kwa ajili ya Kristo, lakini ninyi wenye akili katika Kristo; sisi dhaifu, lakini ninyi hodari; ninyi mna utukufu, lakini sisi hatupati heshima.


(maana anena, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokofu nilikusaidia; tazama, sasa ndio wakati uliokubalika sana; tazama, sasa ndio siku ya wokofu).


wengine walijaribiwa kwa dhihaka na mapigo, naam, kwa mafungo, na kwa kutiwa gerezani:


Bassi na twende kwake nje ya kituo, tukichukua laumu lake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo