Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Matendo 17:3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

3 akiyafunua na kuwaeleza ya kwamba ilimpasa Kristo kuteswa, na kufufuka katika wafu; na ya kama, Yesu huyu ninaewapasha ninyi khabari zake ndiye Kristo.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Aliyaeleza na kuonesha kwamba ilimbidi Kristo kuteswa na kufufuka kutoka kwa wafu. Akawaambia, “Yesu ambaye mimi namhubiri kwenu ndiye Kristo.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Aliyaeleza na kuonesha kwamba ilimbidi Kristo kuteswa na kufufuka kutoka kwa wafu. Akawaambia, “Yesu ambaye mimi namhubiri kwenu ndiye Kristo.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Aliyaeleza na kuonesha kwamba ilimbidi Kristo kuteswa na kufufuka kutoka kwa wafu. Akawaambia, “Yesu ambaye mimi namhubiri kwenu ndiye Kristo.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 akidhihirisha wazi na kuthibitisha kwamba ilikuwa lazima Al-Masihi ateswe na afufuke kutoka kwa wafu. Akasema, “Huyu Isa ninayewaambia habari zake, ndiye Al-Masihi.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 akidhihirisha wazi na kuthibitisha kwamba ilikuwa lazima Al-Masihi ateswe na afufuke kutoka kwa wafu. Akasema, “Huyu Isa ninayewaambia habari zake, ndiye Al-Masihi.”

Tazama sura Nakili

Matendo 17:3
16 Marejeleo ya Msalaba  

Wakaambiana, Je! Mioyo yetu haikuwa ikiwaka ndani yetu, alipokuwa akisema nasi njiani, akitufunulia maandiko?

Akawaambia, Haya ndiyo maneno yangu niliyowaambieni, nilipokuwa kwenu, ya kuwa hayana buddi kutimizwa yote niliyoandikiwa katika torati ya Musa, na katika manabii, na katika zaburi.

Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, na ndivyo ilivyompasa Kristo kuteswa, na kufufuka siku ya tatu;

Kwa maana hawajalifahamu andiko bado, kwamba imempasa kufufuka.

Hatta, akikutana nao, akawaagiza wasitoke katika Yerusalemi, bali waingoje ahadi ya Baba, ambayo mlisikia khabari zake kwangu;

Kwa maana aliwashinda Wayahudi kabisa kabisa mbele ya watu wote, akiwaonyesha kwa maneno ya maandiko ya kuwa Yesu ni Kristo.

Hatta Sila na Timotheo walipotelemka kutoka Makedonia, Paolo akashurutishwa rohoni mwake, akiwashuhudia Wayahudi ya kwamba Yesu ni Kristo.

Lakini mambo yale aliyokhubiri Mungu tangu zamani kwa vinywa vya manabii wake wote, ya kama Kristo atateswa, ameyatimiza hivyo.

Saul akazidi kuwa hodari, akawatia fadhaa Wayahudi waliokaa Dameski, akithubutisha ya kuwa huyu udiye Kristo.

ENYI Wagalatia msio akili, ni nani aliyewaloga, msiisadiki kweli, ninyi ambao Kristo aliwekwa mbele ya macho yemi ya kuwa amesulibiwa?

Tufuate:

Matangazo

Matangazo