Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 17:24 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

24 Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, yeye, kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na inchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono:

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 Mungu, aliyeumba ulimwengu na vyote vilivyomo, ni Bwana wa mbingu na dunia; yeye hakai katika hekalu zilizojengwa na watu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 Mungu, aliyeumba ulimwengu na vyote vilivyomo, ni Bwana wa mbingu na dunia; yeye hakai katika hekalu zilizojengwa na watu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 Mungu, aliyeumba ulimwengu na vyote vilivyomo, ni Bwana wa mbingu na dunia; yeye hakai katika hekalu zilizojengwa na watu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 “Mungu aliyeumba dunia na vyote vilivyomo, ndiye Bwana wa mbingu na nchi; hakai katika mahekalu yaliyojengwa kwa mikono ya wanadamu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 “Mwenyezi Mungu aliyeumba dunia na vyote vilivyomo ndani yake, yeye ndiye Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika mahekalu yaliyojengwa kwa mikono ya wanadamu.

Tazama sura Nakili




Matendo 17:24
36 Marejeleo ya Msalaba  

Wakati ule Yesu akajibu akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na inchi, kwa kuwa uliwaficha haya wenye hekima na busara, ukawafunulia wadogo:


bali mimi nawaambieni, Usiape kabisa; hatta kwa mbingu, kwa maana ndio kiti cha enzi cha Mungu;


Saa ileile Yesu akashangilia katika Roho, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na inchi, kwa kuwa umewaficha wenye hekima na busara mambo haya, ukawafunulia watoto wachanga: Naam, Baba, kwa maana ndivyo vilivyokuwa vinapendeza mbele yako.


MWANZO alikuwako Neno, nae Neno alikuwako kwa Mungu, nae Neno alikuwa Mungu.


Sisi nasi tu wana Adamu hali moja na ninyi; twawakhubiri khabari njema mgenke na kuyaacha mambo haya ya ubatili na kumwelekea Mungu aliye hayi, aliyeumba mbingu na inchi na bahari na vitu vyotc vilivyomo:


Nao waliposikia, wakampaazia Mungu sauti zao kwa moyo mmoja, wakisema, Mola, wewe ndiwe Mungu, ndiwe uliyefanya mbingu na inchi na bahari na vitu vyote vilivyomo:


Illakini yeye aliye juu hakai katika nyumba zilizofanyika kwa mikono, kama vile asemavyo nabii:


Kwa kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana ni dhahiri ndani yao, kwa maana Mungu aliwadhihirishia.


mwisho wa siku bizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi yote, kwa yeye aliufanya ulimwengu.


Maana killa nyumba imetengenezwa na mtu; illa yeye aliyevitengeneza vitu vyote ni Mungu.


Nikaona kiti eba enzi, cheupe, kikubwa, nae aketiye juu yake; inchi na mbingu zikakimbia nso wake, na mahali pao hapakuonekana.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo