Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 17:22 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

22 Paolo akasimaina katikati ya Areopago, tikasema, Enyi watu wa Athene, katika mambo yote naona ya kuwa ninyi ni watu wa kutafakari sana mambo ya dini.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Basi, Paulo alisimama mbele ya baraza la Areopago, akasema, “Wananchi wa Athene! Ninaona kwamba nyinyi, kwa vyovyote, ni watu wa dini sana,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Basi, Paulo alisimama mbele ya baraza la Areopago, akasema, “Wananchi wa Athene! Ninaona kwamba nyinyi, kwa vyovyote, ni watu wa dini sana,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Basi, Paulo alisimama mbele ya baraza la Areopago, akasema, “Wananchi wa Athene! Ninaona kwamba nyinyi, kwa vyovyote, ni watu wa dini sana,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 Ndipo Paulo akasimama katikati ya mkutano wa Areopago, akasema, “Enyi watu wa Athene! Ninaona kwamba katika kila jambo ninyi ni watu wa dini sana.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 Ndipo Paulo akasimama katikati ya Areopago akasema, “Enyi watu wa Athene! Ninaona kwamba katika kila jambo ninyi ni watu wa dini sana.

Tazama sura Nakili




Matendo 17:22
8 Marejeleo ya Msalaba  

Nao walimsindikiza Paolo wakampeleka hatta Athene; na wakiisha kupokea maagizo kuwapelekea Sila na Timotheo, ya kama wasikawie kumfuata, wakaenda zao.


Paolo alipokuwa akiwangojea katika Athene akaona jinsi mji ule ulivyojaa sanamu, roho yake ilichukizwa sana ndani yake.


Wakamshika, wakamchukua hatta Areopago, wakisema, Je, twaweza kujua maana ya elimu hii mpya inenwayo nawe?


Baadhi ya wanaume wakashikamana nae, wakaamini; katika hao alikuwamo Dionuso, Mwareopago, na mwanamke mmoja jina lake Damari, na watu wengine pamoja na hao.


Na karani wa mji alipokwisha kuwatuliza watu, akasema, Enyi wanaume wa Efeso, ni mtu gani asiyejua ya kuwa mji wa Efeso ni mtunzaji wa hekalu ya Artemi, mungu mke aliye mkuu, na wa kitu kile kilichoanguka kutoka mbinguni?


hali walikuwa na maswali juu yake katika dini yao wenyewe, na katika khabari ya mtu mmoja Yesu, aliyekuwa amekwisha kufa, ambae Paolo alishika kusema kwamba yu hayi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo