Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Matendo 17:18 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

18 Na baadhi ya Waepikurio na Wastoiko, matilosofo, wakakutana nae. Wengine wakasema, Mtu huyu mwenye maneno mengi anataka kusema nini? Wengine walisema, Anaonekana kuwa mtangaza khabari za miungu migeni, kwa maana alikuwa akikhubiri khabari za Yesu na ufufuo.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Wengine waliofuata falsafa ya Epikuro na Stoiki walibishana naye. Wengine walisema, “Anataka kusema nini huyu bwanamaneno?” Kwa kuwa Paulo alikuwa anahubiri juu ya Yesu na juu ya ufufuo, wengine walisema, “Inaonekana kama anahubiri juu ya miungu ya kigeni.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Wengine waliofuata falsafa ya Epikuro na Stoiki walibishana naye. Wengine walisema, “Anataka kusema nini huyu bwanamaneno?” Kwa kuwa Paulo alikuwa anahubiri juu ya Yesu na juu ya ufufuo, wengine walisema, “Inaonekana kama anahubiri juu ya miungu ya kigeni.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Kundi la wenye falsafa, Waepikureo na Wastoiko, wakajibizana naye. Baadhi yao wakasema, “Je, huyu mpayukaji anajaribu kusema nini?” Wengine wakasema, “Inaonekana anasema habari za miungu ya kigeni.” Walisema haya kwa sababu Paulo alikuwa anahubiri Injili kuhusu Isa na ufufuo wa wafu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Kisha baadhi ya Waepikureo na Wastoiko wenye falsafa wakakutana naye. Baadhi yao wakasema, “Je, huyu mpayukaji anajaribu kusema nini?” Wengine wakasema, “Inaonekana anasema habari za miungu ya kigeni.” Walisema haya kwa sababu Paulo alikuwa anahubiri habari njema kuhusu Isa na ufufuo wa wafu.

Tazama sura Nakili

Matendo 17:18
16 Marejeleo ya Msalaba  

Hatta alipowafikia wanafunzi wake, akaona makutano mengi wakiwazunguka na waandishi wakijadiliana nao;

Alipokuwa akiwaambia haya, waandishi na Mafarisayo wakaanza kumsonga vibaya, na kumchokoza kwa masiala mengi, wakimwotea,

ya kwamba Kristo hana buddi kuteswa na ya kwamba yeye kwanza kwa kufufuliwa katika wafu atatangaza khabari za nuru kwa watu wake na kwa watu wa mataifa.

wakifadhaika sana kwa sababu wanawafundisha watu na kuukhubiri ufufuo wa wafu unaopatikana kwa Yesu.

Na killa siku ndani ya hekalu na nyumbani mwao, hawakuacha kufundisha na kukhubiri khabari njema za Yesu kwamba ni Kristo.

Lakini baadhi ya watu wa sunagogi lililokwitwa sunagogi la Malibertino, na la Wakurene na la Waiskanderia, na la wale wa Kilikia na Asia, wakaondoka wakajadiliana na Stefano:

wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika,

Mtu asijidanganye nafsi yake: kama mtu akijiona kuwa mweuye hekima kati yeuu katika dunia hii, na awe mpumbavu, apate kuwa mwenye hekima.

Sisi tu wapumbavu kwa ajili ya Kristo, lakini ninyi wenye akili katika Kristo; sisi dhaifu, lakini ninyi hodari; ninyi mna utukufu, lakini sisi hatupati heshima.

Angalieni intu asiwateke kwa filosofia yake na madanganya matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wana Adamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo