Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Matendo 17:13 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

13 Lakini Wayahudi wa Thessaloniki walipopata khabari ya kwamba Neno la Mungu linakhubiriwa na Paolo katika Beroya, wakaenda huko wakawachafua makutano.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Lakini, Wayahudi wa Thesalonike walipogundua kwamba Paulo alikuwa anahubiri neno la Mungu huko Berea, walikwenda huko, wakaanza kufanya fujo na kuchochea makundi ya watu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Lakini, Wayahudi wa Thesalonike walipogundua kwamba Paulo alikuwa anahubiri neno la Mungu huko Berea, walikwenda huko, wakaanza kufanya fujo na kuchochea makundi ya watu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Lakini, Wayahudi wa Thesalonike walipogundua kwamba Paulo alikuwa anahubiri neno la Mungu huko Berea, walikwenda huko, wakaanza kufanya fujo na kuchochea makundi ya watu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Lakini wale Wayahudi wa Thesalonike waliposikia kuwa Paulo anahubiri neno la Mungu huko Beroya, wakaenda huko ili kuwashawishi watu na kuwachochea.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Lakini wale Wayahudi wa Thesalonike waliposikia kuwa Paulo anahubiri neno la Mungu huko Beroya, wakaenda huko ili kuwashawishi watu na kuwachochea.

Tazama sura Nakili

Matendo 17:13
14 Marejeleo ya Msalaba  

Ole wenu waandisbi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mnakula nyumba za wajane, na kwa unafiki mnasali sala ndefu; kwa hiyo mtapokea hukumu iliyo kubwa mno.

Je! wadhani kwamba nimekuja niipe dunia amani? Nawaambieni, Sivyo, bali mafarakano.

Walakini Wayahudi wasioamini wakawataharakisha watu wa mataifa na kuwatia nia mbaya juu ya ndugu.

WAKIISHA kupita kati ya Amfipoli na Apollonia wakafika Thessalonika, na hapo palikuwa na sunagogi la Wayahudi.

Marra ndugu wakawapeleka Paolo na Sila usiku hatta Beroya. Walipofika huko wakaingia katika sunagogi la Wayahudi.

Na Wayahudi wasioamini wakaona wivu, wakajitwalia watu kadha wa kadha katika watu ovyo wasio na sifa njema wakakutanisha mkutano, wakafanya ghasia mjini, wakawaendea watu wa nyumba ya Yason wakataka kuwapeleka mbele ya watu wa mji;

Watu hawa wakafuataua nae mpaka Asia, Sopater Mberoya, na Aristarko na Sekundo, watu wa Thessalonika, na Gayo mtu wa Derbe, na Tukiko na Trofumo watu wa Asia.

Bassi zile siku saba zilipokuwa karibu kutimizwa, Wayahudi waliotoka Asia wakamwona ndani ya hekalu, wakawataharakisha watu wote, wakamkamata, wakapiga kelele, Enyi wanaume wa Israeli, saidieni.

Wakawataharakisha watu na wazee na waandishi: wakaniwendea, wakamkamata, wakampeleka mbele ya baraza.

kwa kusafiri marra nyingi; khatari za mito; khatari za wanyangʼanyi; khatari kwa jamaa; khatari kwa mataifa; khatari za mijini; khatari za jangwani; khatari za baharini; khatari kwa ndugu za uwongo;

Tufuate:

Matangazo

Matangazo