Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 17:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 WAKIISHA kupita kati ya Amfipoli na Apollonia wakafika Thessalonika, na hapo palikuwa na sunagogi la Wayahudi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Kwa kupitia Amfipoli na Apolonia, walisafiri mpaka Thesalonike ambako kulikuwa na sunagogi la Wayahudi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Kwa kupitia Amfipoli na Apolonia, walisafiri mpaka Thesalonike ambako kulikuwa na sunagogi la Wayahudi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Kwa kupitia Amfipoli na Apolonia, walisafiri mpaka Thesalonike ambako kulikuwa na sunagogi la Wayahudi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Wakasafiri kupitia Amfipoli na Apolonia wakafika Thesalonike, ambako kulikuwa na sinagogi la Wayahudi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Wakasafiri kupitia Amfipoli na Apolonia wakafika Thesalonike, ambako kulikuwa na sinagogi la Wayahudi.

Tazama sura Nakili




Matendo 17:1
13 Marejeleo ya Msalaba  

IKAWA huko Ikonio wakaingia pamoja katika sunagogi ia Wayahudi, wakanena; hatta jamaa kubwa ya Wayahudi na ya Wayunani wakaamini.


Kwa maana tangu zamani za kale Musa anao watu wakhubirio mambo yake; katika killa mji husomwa killa siku katika masunagogi.


Hatta siku ya sabato tukatoka nje ya lango, tukaenda kando ya mto, tukidhani ya kuwa hapo pana mahali pii kuomba; tukaketi, tukasema na wanawake waliokutana pale.


Marra ndugu wakawapeleka Paolo na Sila usiku hatta Beroya. Walipofika huko wakaingia katika sunagogi la Wayahudi.


Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thessaloniki, kwa kuwa walilipokea Neno kwa uelekefu wa moyo, wakayachunguza maandiko, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo.


Lakini Wayahudi wa Thessaloniki walipopata khabari ya kwamba Neno la Mungu linakhubiriwa na Paolo katika Beroya, wakaenda huko wakawachafua makutano.


Watu hawa wakafuataua nae mpaka Asia, Sopater Mberoya, na Aristarko na Sekundo, watu wa Thessalonika, na Gayo mtu wa Derbe, na Tukiko na Trofumo watu wa Asia.


Tukapanda katika merikebu ya Adramuttio iliyokuwa tayari kusafiri hatta miji ya pwani za Asia, tukatweka; Aristarko, Mmakedoni wa Thessalonika, akiwa pamoja nasi.


Kwa kuwa hatta katika Tʼhessaloniki mliniletea msaada kwa mahitaji yangu wala si marra moja tu.


PAOLO, na Silwano, na Timotheo, kwa kanisa la Wathessaloniki, katika Mungu Baba, na Bwana Yesu Kristo. Neema na iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.


bali tukiisha kuteswa kwanza na kutendwa jeuri, kama mjuavyo, katika Filippi, twalithubutu katika Mungu kuinena Injili ya Mungu kwenu, kwa kuishindania sana.


PAOLO, Silwano, na Timotheo kwa kanisa la Wathessaloniki lililo katika Mungu Baba yetu, na Bwana Yesu Kristo:


maana Dema aliniacha, akiupenda ulimwengu wa sasa, akasafiri kwenda Thessaloniki; Kreske Galatia, Tito Daimatia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo