Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 16:5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

5 Makanisa yakatiwa nguvu kwa imani, hesabu yao ikaongezeka killa siku.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Hivyo, yale makanisa yalizidi kuwa imara katika imani, na idadi ya waumini ikaongezeka kila siku.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Hivyo, yale makanisa yalizidi kuwa imara katika imani, na idadi ya waumini ikaongezeka kila siku.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Hivyo, yale makanisa yalizidi kuwa imara katika imani, na idadi ya waumini ikaongezeka kila siku.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Hivyo makundi ya waumini yakaimarika katika imani, na wakaongezeka kwa idadi kila siku.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Hivyo makundi ya waumini yakawa imara katika imani na kuongezeka kiidadi kila siku.

Tazama sura Nakili




Matendo 16:5
23 Marejeleo ya Msalaba  

Mkono wa Bwana ukawa pamoja nao: watu wengi wakaamini, wakamwelekea Bwana.


Neno la Bwana likazidi na kuenea.


Akapita katika Shami na Kilikia akawatia moyo makanisa.


wakimsifu Mungu, na kuwapendeza wutu wote. Bwana akalizidisha kanisa killa siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.


Lakini wengi katika hao waliosikia lile neno waliamini: na hesabu ya watu ilikuwa kama elfu tano.


waamini wakazidi kuja kwa Bwana, wengi, wanaume ha wanawake:


Nenu la Mungu likaenea: hesahu ya wanafunzi ikazidi sana katika Yerusalemi: jamii kubwa la makuhani wakaitii Imani.


Bassi makanisa wakapata raha katika Yahudi yote na Galilaya na Samaria, wakajengewa, wakiendelea katika kicho cha Bwana, na faraja ya Roho Mtakatifu.


Sasa na atukuzwe yeye awezae kutufanya imara kwa injili yangu na kwa kukhubiriwa Yesu Kristo, kwa ufunuo wa ile siri iliyostirika tangu zamani za milele,


Bassi, ndugu wapendwa, mwe imara, msiotikisika, mkizidi sana kutenda kazi ya Bwana siku zote, kwa kuwa taabu yenu siyo burre katika Bwana.


KRISTO alitufanya huru kwa uhuru; bassi, simameni, msinaswe tena kwa kifungo cha utumwa.


Bassi kama mlivyompokea Kristo Yesu, Bwana, enendeni vivyo hivyo katika yeye,


apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwaua wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote.


tukamtuma Timotheo ndugu yetu, mtumishi wa Mungu, mfanya kazi pamoja naswi katika Injili ya Kristo, kuwafanya ninyi imara na kuwafariji kwa ajili ya imani yenu,


Na Bwana wetu Yesu Kristo, na Mungu Baba yetu aliyetupenda akatupa faraja ya milele na tumaini jema, katika neema,


Msichukuliwe na mafundisho ya namna nyingine nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa neema, wala si kwa vyakula, ambavyo wao waliokwenda navyo bawakupata faida.


Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, atawathubutisha, atawatia nguvu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo